Marehemu, Mez B enzi za uhai wake.

Aliyewahi kuwa memba wa kundi la Chamber Squad, Moses Bushagama ‘Mez B’ ambaye amefariki jana mjini Dodoma anatarajiwa kuzikwa Jumatatu katika makaburi ya Wahanga yaliopo Maili Mbili mjini Hapo. Mtandao huu uliongea na mama wa marehemu, Marry Mkandawile ambaye alisema kuwa kwa sasa msiba upo maeneo ya Kisasa mjini hapo.

Msanii Mez B aliyekuwa akiwika na kundi la Chamber Squad, Moses Bushagama ‘Mez B’ amefariki dunia asubuhi ya leo majira ya saa 4:30 mjini Dodoma.

Hii imekuwa ni pigo la pili kwa kundi la Chamber Squad kupoteza memba wake baada ya awali kumpoteza Albert Mangweha ‘Ngwear’.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: