Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication, Francis Nanai, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 13, 2015 kwa mazungumzo na kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo. Kushoto ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bakari Machumu. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Uongozi wa juu wa Kampuni ya Mwananchi Communication, Mkurugenzi Mtendaji Francis Nanai (katikati) na Mhariri Mtendaji wa Kampuni hiyo, Bakari Machumu, wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Feb 13, 2015 kwa mazungumzo na kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo na kuelezea kazi zinazofanywa na kampuni hiyo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa juu wa Kampuni ya Mwananchi Communication, Mkurugenzi Mtendaji Francis Nanai (wa pili kushoto) Mhariri Mtendaji Bakari Machumu (kulia) na Mshauri wa Kampuni hiyo, Teddy Mapunda (kushoto) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo, Feb 13, 2015. Picha na OMR
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: