Bondia Iddi Bonge kushoto akitunishiana misuli na Alphonce mchumiatumbo baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika feb 14 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba Dar es Salaam siku ya Jumamosi. Picha na SUPER D.
Na Mwandishi Wetu.
Mabondia wa uzito wa juu wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa taifa mabondia hawo ni Iddi Bonge na Alphonce Mchumiatumba ambao watapanda uringoni siku ya Feb 14 katika ukumbi wa P.T.A sabasaba kwa ajili ya kumaliza ubishi ambao umetanda mitaani 'Ni nani Bingwa wa Uzito wa juu nchini'.
Mpambano huo wa raundi kumi utakuwa ni wa aina yake kwa kuwa kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: