Wapendwa tunapoendelea na kipindi hiki kwa Kwaresima, nawaalika tuangalie sehemu ya Neno la Mungu - Injili ya Luka 6:29-30
Lugha tunayotumia kuzungumza juu ya mahusiano yetu na Mungu inaweza kuwa ya mapambo na ya kupendeza, uhalisi wa kuishi mahusiano hayo ni wa aina moja tu - nao tunasema: "Pendaneni !" Hii haimaanishi kujisikia vizuri kuwa na urafiki na watu wengine au ndugu wa karibu, bali kupenda katika roho na kweli na kwa uhakika.
Kupenda ni kuchagua kwa makusudi maslahi ya mwingine juu ya maslahi yangu kwa kadiri inayowezekana (the spirit of lent is a radical choice to love).
Kumpenda mwingine ni uamuzi wangu thabiti wa kufunga kula ili mwingine ale, kuacha matumizi yangu kadhaa ili mwingine aishi, kuacha tabia yangu fulani mbaya ili nami nijue kumsamehe mwingine. Yesu yupo wazi kabisa na anamaanisha anachosema: "Akikupiga shavu moja, mgeuzie jingine; akitaka shati, mpe na koti pia; akitaka uende maili moja, nenda naye mbili." (Lk 6:29-30).
Maneno haya ya Yesu sio ya kudharau kwani Paulo ametuambia : "Kwa sababu neno la Msalaba kwao wnaopotea ni upuuzi. Bali kwetu tunaoamini na kuokolewa, ni Nguvu ya Mungu." (1Kor 1:18)
Katika maisha yetu ya Kwaresima na hata nje ya Kwaresima kuna wengi watakaotuudhi. Tubebe basi sura na moyo wa Kristu ambaye hakujibu kwa tukano pale alipopigwa na kutemewa mate. Yeye alikaa kimya na kuwaombea - "Baba, usiwahesabie dhambi hii.."
Tuziombee familia zenye magomvi yasiyoisha, tuziombee koo na wana ndugu hata Wakristu wasiosalimiana. Tusali kwa ajili ya nchi zilizo katika vita na mapigano.
Muwe na siku njema sana.
Jumapili iwe njema kwako pia familia. Na ahsante kwa neno!
ReplyDelete