*MKULIMA, MWALIMU WASHINDA MAGARI YA AIRTEL YATOSHA ZAIDI
Mkulima toka mkoani Pwani Ramadhani Dilunga miaka 53 na Mwalimu mstaafu wa Mtwara bw, Namtapika Kilumba (60) ni miongoni mwa Watanzania watatu walioibuka washindi kwenye droo ya kwanza ya Airtel Yatosha Zaidi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Washindi hao kila mmoja ameibuka mshindi wa gari aina ya IST Toyota mpya, ikiwa ni siku chache tu tangu kuzindulia kwa promosheni hiyo.
Airtel Tanzania wiki iliyopita ilitangaza dhamira yake ya kuwazawadia wateja wake wanaojiunga na bando za Airtel Yatosha gari moja kila siku kwa siku 60 ambapo mwishoni mwa wiki tayari magari matatu yalipata washindi.
Balozi wa promosheni ya Airtel Yatosha zaidi na msanii nyota wa Bongo Movie, Elizabeth Michael 'Lulu' akiwasiliana kwa simu na mmoja wa washindi wa promosheni ya ‘Airtel Yatosha Zaidi’, katika droo iliyochezwa katika Makao Makuu ya Airtel Tanzania jijini Dar es Salaam jana, ambapo wateja watatu wa mtandao huo, Namtapika Seif Kilumba wa Mtwara, Ramadhan Mohamed Dilunga wa Kimanzichana Pwani na Mwajabu Omari Churian wa Manzese jijini, waliibuka washindi na kutwaa gari aina ya Toyota IST kila moja. Anayeshuhudia (kushoto) ni Mkaguzi Mwandamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid.
---Balozi wa Airtel, na msanii maarufu wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, ndiye aliyekuwa na jukumu la kuwapigia simu washindi na kuwapa taarifa hizo nzuri kwa mwaka 2015 chini ya Mkaguzi Mwandamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid
Wa kwanza kupigiwa alikuwa Namtapika Kilumba wa Mtwara mwenye umri wa miaka 60 na aliposikia sauti ya Lulu ikisema; “Ninapenda kukutaarifu kuwa umeshinda gari aina ya IST Toyota mpya baada ya kujiunga na Airtel Yatosha Zaidi”, alipiga kelele kwa furaha na mara moja akamshukuru Mungu pamoja na Lulu.
“Mungu wangu. Sikutarajia kabisa kama leo ningepata taarifa nzuri kama hizo! Kumbe ni kweli kuwa mtu yeyote anaweza kushinda promosheni ya Airtel? siamini,” alisema … kwa njia ya simu; na hata wengine pia waliopigiwa simu na Lulu walikuwa na maoni yanayoshabihiana na hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya droo hiyo, Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando, alisema: “Haya ndio kwanza magari matatu tu. Bado mengine 57 yote aina ya IST Toyota mapya kabisa yapo ‘showroom’. Ndani ya 60 za mwaka huu, wateja 60 wa Airtel watakuwa wakiishi maisha mapya katika dunia ya ndoto zao.
“Watakuwa ni wamiliki wa magari kwa kujiunga na bado za Airtel Yatosha zaidi kwa kupiga simu *149*99# na kujiunga. Hebu fikiria, unapata muda wa maongezi zaidi, vifurushi vya internet zaidi, SMS zaidi na bado unakuwa na nafasi ya kujishindia gari.”
Mmbando alimtaja mshindi mwingine kuwa ni Mwajabu Churian mwenye umri wa miaka 27 na mfanyabiashara anaeishi Mbagala huku akiwasihi wateja wa Airtel kuendelea kufurahia huduma hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: