• Viingilio shilingi elfu 15 kwenye vituo na elfu 20 mlangoni
Tamasha la miaka kumi ya THT litakalofanyika jumamosi hii katika viwanja vya Escape 1 Mikocheni, limekamilisha maandalizi yake na hivyo kuwataka wadau na wapenzi wake wajitokeze kwa wingi kushuhudia burudani kubwa ya mziki hapa nchini.
THT, ambayo inasifika kwa kuzalisha wasanii mahiri nchini kama Linah, Barnaba, Mwasiti, Ditto, Mataluma, Vumi, Beka, Recho, Marlaw, Msami, Makomando na wengine wengi, imejipanga kutoa burudani kubwa ya mziki kwa mashabiki wake.
Akizungumza kuhusu maandalizi hayo, Meneja Mkuu wa THT, Mwita Mwaikenda alisema maandalizi yanaenda vema na mashabiki wahudhurie kwa wingi kujionea namna kituo hicho kilivyoweza kufanya mapinduzi kwenye tasnia ya muziki.
‘Mpaka sasa wasanii wa THT watakaotoa burudani wako tayari, na kama mnavyojua THT utamaduni wake ni kupiga muziki kwa kutumia bendi lakini pia wasanii watakaotusindikiza ni kama Ben Paul, Mrisho Mpoto na Weusi’ alisema Mwita.
Akizungumzia wadhamini waliojitokeza kwenye shughuli hiyo, Mwita aliwashukuru Mr. Price waliowavisha wasanii wote, Mziiki.Com ya Spice Afrika walionunua tiketi 500 za tamasha kwa ajili ya wateja wao, SanMoto Pikipiki waliotoa pikipiki, Tanzania Fashion and Design Limited, Darling Hair ambao wametoa nywele kwa waimbaji wote wa kike na Clouds Media Group.
‘Tunatoa shukrani za dhati kwa wadhamini wetu, kwa kutuunga mkono katika kuadhimisha miaka kumi ya kuleta mapinduzi katika burudani’ alisema Mwita.
Tiketi za tamasha zinapatikana maduka ya Robby One Fashion Kinondoni na Sinza, Yahya Boutique Kinondoni, Born 2 Shine Mwenge, Ofisi za Clouds, Moca City Samora Avenue, City Sports Lounge, Mr Price na THT Kinondoni.
Kiingilio ni 15,000/- kwenye vituo hivyo na kwa wale wanaotaka za VIP ni 50,000/- na zinapatikana THT pekee yake. Siku ya onyesho pale Escape One, mlangoni kiingilio kitakuwa ni Shs 20,000/=.
Toa Maoni Yako:
0 comments: