Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya TIMAMU AFRICAN MEDIA, Timoth Corard Kachumia (TICO) -(katikati) akiongea mbele ya waandishi wa Habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo wakati akitambulisha wasanii wanaoingia kambini wiki ijayo kwa ajili ya filamu mpya inayotarajiwa kuchezwa hivi karibuni.
Mkurugenzi Msaidizi wa Kampuni ya TIMAMU AFRICAN MEDIA, Dorice Kaizilege akiongea mbele ya waandishi wa Habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo wakati akitambulisha wasanii wanaoingia kambini wiki ijayo kwa ajili ya filamu mpya inayotarajiwa kuchezwa hivi karibuni.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya TIMAMU AFRICAN MEDIA, Timoth Corard Kachumia (TICO) akihojiwa na waandishi wa habari kuhusu ushindi wa tuzo ya Dogo Masai iliyopata tuzo nchini Marekani hivi karibuni, Silicon Valley African Film Festival .
Wasanii wanatakaoinhia kambini hivi karibuni.
Timamu African media ni kampuni ya uandaaji na utengenezaji wa filamu, ilianzishwa mwaka 2008 ambapo tangu kuanzishwa kwa kempaka sasa imeshaandaa na kutengeneza filamu 15.
Baadhi ya filamu hizo zimeandaliwa na waandaji ndani ya kampuni na zingine zimeandaliwa na producers wengine kutoka nje ya kampuni ambao wamekuwa wakitumia crew pamoja na vifaa vya kampuni hii katika kuandaa na kutengneza filamu zao.
Filamu tano kati ya filamu zilizoandaliwa na kampuni hii zimefanikiwa kunyakua award kutoka sehemu mbalimbali nchini pamoja na nje ya nchi. Filamu hizo ni;-
Mdundiko – imeonyeshwa na kushinda tuzo kutoka silicon valley African film festival ambazo zinafanyika san fransisco nchini Marekani - 2013
DogoMasai – imeonyeshwa na kushinda tuzo kutoka silicon valley African film festival ambazo zinafanyika san fransisco nchini Marekani – 2014
C.I.D – imeshinda tuzo ya filamu bora ya action nchini Tanzania kupitia tuzo za Action and Cut viewers Choice Awards – 2014
Kisate – Main character Jackson Kabirigi amefanikiwa kunyakua tuzo katika kipengele cha Best Actor – 2014
Nguvu ya imani – Editor wa Filamu Timoth Conrad amefanikiwa kunyakua tuzo ya editor bora wa Filamu nchini Tanzania – 2014
Hatia - Editor wa filamuTimoth Conrad amefanikiwa kunyakua tuzo ya editor bora wa filamu nchini Tanzania – 2014
Pia Timamu African Media imeanzisha kitu kinachoitwa Timamu African Film Festival (TAFF) ambayo itafnyika nchini Tanzania mwezi wa 9 mwaka huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: