Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akitoa taarifa ya mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi Desemba, 2014. Kulia ni Meneja Utafiti wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Johnson Nyella na Meneja Idara ya Ajira na Bei, Ruth Minja.
Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akitoa taarifa ya mfumuko wa bei wa taifa wa mwezi Desemba, 2014. Kulia ni Meneja Utafiti wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Johnson Nyella.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Dotto Mwaibale
MKURUGENZI wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka, Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraim Kwesigabo alisema mfumuko wa bei wa taifa kutoka Januari hadi Desemba mwaka jana umepungua hadi asilimia 6.1 kutoka wastani wa asilimia 7.9, mwaka 2013.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kwesigabo alisema kupungua kwa wastani huo kulichangiwa na kupungua kwa kasi ya kupanda bei ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula.
Alisema wastani wa mfumuko wa bei ambao hujumuisha vyakula na nishati umepungua karibu nusu mwaka 2014 kutoka asilimia 6.2 kwa mwaka 2013.
Pia alisema kupungua kwa mfumuko wa bei wa mwaka 2104 kunamaanisha, kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka 2014 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo mwaka 2013.
Kuhusu mfumuko wa bei wa taifa kwa mwezi Desemba 2014 umepungua hadi asilimia 4.8 kutoka asilimia 5.8 ilivyokuwa mwezi Novemba 2014. Hiyo ni kutokana na upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha.
Kwa upande wake Meneja Utafiti wa Biashara kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Johnson Mnyella alisema moja kati ya malengo ya benki hiyo ni kuwa na mfumko wa bei kati ya asilimia 5, hivyo wamefanikiwa kufikia pale wanapopataka.
Mnyella alisema benki hiyo imekuwa ikiunga mkono jitihada mbalimbali pindi inapotokea mfumuko wa bei na wamekuwa wakifanikiwa huku akisisitiza kuwa kutokana na kuwepo kwa uzalishaji mkubwa wa chakula na mfumko wa bei utaendelea kuwa chini.
Toa Maoni Yako:
0 comments: