Nimesoma katika gazeti la Habari leo la tarehe 9 Januari,2015,toleo la 02942,Ukurasa wa 8 habari na mwandishi Prisca Libaga,Arusha ,habari yenye kichwa cha habari "Mradi wa Maji wadaiwa kutoa Tope".

Mwandishi amenukuu malalamiko ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Onesmo Nangoro akiongea kwenye kikao cha Kamati ya ushauri mkoa (RCC) kilichofanyika juzi kuwa mimi Amos Makalla,Naibu Waziri wa Maji nilidanganywa nikazindua mradi wa maji wilaya ya Longido uliogharimu shilingi milioni 300 na kwamba mradi huo uliwekwa tanki la bandia na sasa mradi huo unatoa tope na siyo maji.

Naomba nitumie fursa hii kukanusha habari hiyo kuwa siyo ya kweli mimi kama naibu waziri maji sijafanya ziara wilayani Longido na umma uelewe sijawahi kuzindua mradi unaotajwa.

Aidha nimekuwa na ziara mkoa wa Arusha kuanzia tarehe 15 desemba hadi 18 mwaka jana kwa kutembelea wilaya ya Karatu,Arusha jiji, halmashauri Arusha Dc na Meru na ieleweke kuwa wilaya ya Longido zikufanya ziara tarehe 19 kutokana na maombi ya mkuu wa wilaya na mbunge wa Longido kuniomba nihairishe wilaya yao kutokana na wilaya kuwa na mgeni wa kitaifa ni hivyo waliniomba niwapangie wakati mwingine.

Hivyo kauli ya mwenyekiti wa mkoa ilichukuliwe kuwa waliompatia habari hizo kuwa mimi nilizindua mradi wamempotosha na si za kweli.

Mwisho wizara yangu imepokea taarifa hii na itaifanyia kazi ili kuona mradi huo unatekelezwa kwa kiwango kinachotakiwa na niwaombe wananchi wa Longido wawe watulivu wakati jambo hili linashughulikiwa.

Amos G Makalla(mb)
Naibu waziri maji
9 Januari, 2015
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: