Kamishna Jenerali wa Magereza, John Minja, akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumpandisha cheo koplo, Catherina Lange kuwa Sanjenti wa Jeshi la Magereza.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Minja, akimpandisha
cheo Koplo Catherine Lange, kuwa Sajenti wa Jeshi la Magereza baada ya kung’ara katika mashindano mbalimbali ya kimataifa ya riadha yaliyofanyika katika nchi za Brazil, China na Angola.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Minja, akimpandisha
cheo Koplo Catherine Lange, kuwa Sajenti wa Jeshi la Magereza baada ya kung’ara katika mashindano mbalimbali ya kimataifa ya riadha yaliyofanyika katika nchi za Brazil, China na Angola.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Minja, akipompongeza
mwanariadha, Catherina Lange baada ya kumpandisha cheo.
Catherina Lange.
Catherina Lange akiwa amepozi.
Na Mwandishi Wetu.
KAMISHINA Jenerali wa Magereza (CGP), John Minja, leo amempandisha cheo mwanariadha wa mbio ndefu, Catherina Yuku kutoka cheo cha CPL wa Magereza hadi SGT wa Jeshi hilo kutokana na juhudi binafsi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akimpandisha cheo hicho, Minga alisema ni kutokana na umahiri wake katika mchezo huo tangu aanze kupata mialiko ya kushiriki mashindano ya kimataifa kupitia Riadha Tanzania (RT) tangu mwaka 2011.
Alisema kwa mamlaka aliyonayo katika Jeshi hilo wa mujibu wa sheria ya Magereza ya mwaka 1997, kwa ushindi na sifa alizoliletea Jeshi la Magereza na Taifa, anampandisha hadi ngazi hiyo katika kutambua na kuthamini juhudi yake.
Alisema, mwanariadha huyo ameshiriki mashindano ya Kimataifa mara 12 ambapo yalifanyika katika nchi za Brazil, China, Angola na mikoa mbalimbali hapa nchini.
CGP Minja alisema mwanariadha huyo ana rekodi ya kupata medali tisa; tatu za dhahabu, tatu za fedha na tatu za shaba na katika mashindano ambayo hajapata medali, bado alishika nafasi ya nne na ya tano akipata medali za ushindi.
“Mashindano aliyoshiriki yalishirikisha wanaraidha kuanzia 95 hadi 23, 657, kiwango chake kinazidi kupanda kwani katika mashindano ya Desemba 2014 yaliyofanyika Shanghai, China alishika nafasi ya kwanza kati ya washiriki 23, 657 na katika Uhuru Marathon ya jijini Dar es Salaam Desemba mwaka jana, alishika nafasi ya kwanza kati ya washiriki 520,” alisema.
Kwa upande wake, Catherina alisema kuwa anaushukuru uongozi wa Magereza kwa kuthamini na kutambua mchango wake.
“Zawadi hii itanifanya nizidi kuongeza juhudi katika mchezo huu, najisikia faraja sana kupewa kitu kama hiki na nawahaidi kwamba zawadi hii itanifanya niendelee kufanya vizuri,” alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments: