Meneja Mkuu wa Fastjet wa kanda ya Afrika Mashariki, Jimmy Kibati (kushoto), akiwa na Grace Makazi ambaye alipokea ofa ya tiketi mbili za bure kama abiria wa milioni moja wa shirika hilo la ndege mara baada ya kutua jijini Dar es Salaam juzi, Shirika la Fastjet limetoa tiketi mbili za bure kwenda na kurudi mahali popote ndani ya nchi kwa abiria wake wa millioni moja.
Meneja Mkuu wa Fastjet wa kanda ya Afrika Mashariki, Jimmy Kibati akiwa kwenye picha ya pamoja na Grace Makazi na wafanyakazi wa Fastjet.
Meneja Mkuu wa Fastjet wa kanda ya Afrika Mashariki, Jimmy Kibati akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Fastjet mara baada ya kuwasili kwa mteja wa millioni moja wa shirika hilo bi. Grace Makazi.
Na Mwandishi Wetu.
Fastjet shirika la ndege la gharama nafuu limesafirisha abiria wake wa milioni moja, ndani ya kipindi cha miaka miwili tangu shirika hili inayofanya masafa yake Afrika kuzinduliwa.
Mteja huyo aliyebahatika, Grace Makazi, akiongozana na mtoto wake Marieta alisafiri kutoka Mbeya kwenda Dar es Salaam katika ndege aina ya Airbus A319. Kuadhimisha mafanikio hayo, abiria huyo alipotua alikutana na Meneja Mkuu wa Fastjet kwa kanda ya Afrika Mashariki Bw. Jimmy Kibati, pamoja na wafanyakazi wengine kutoka kwenye shirika hilo.
Alipofika jijini Dar es Salaam abiria huyo aliyeonekana akiwa na furaha, ambaye alikuwa amepanda shirika hilo kwa mara ya pili, alisema, “Kitendo cha kukutana na wafanyakazi wa Fastjet kama abiria wao wa milioni moja ilikuwa yakipekee sana.”
Bi. Makazi, ambaye ni askari polisi kutoka jijini Dar es Salaam, alisafiri kwenda mbeya kuwatembelea wazazi wake huku akitumia ndege ya Fastjet ambayo inasafiri mara mbili kwa wiki kati ya makao makuu ya biashara ya nchi na ‘mji huo wa kijani’. Hapo awali alikuwa anategemea kupanda basi na kusafiri umbali wa kilometa 870.
“Kusafiri kwa basi kulikuwa kuna chosha sana lakini sasa ninaweza nikapanda Fastjet. Ninafuraha kubwa sana kutumia shirika hili la ndege, safari zao za gharama nafuu ina maanisha kwamba abiria wengi zaidi wanaweza wakasafiri kwenda sehemu tofauti tofauti,” alisema Grace.
Fastjet inatoa huduma ya safari za ndani na nje kwa wastani ya mara saba kwa siku.
Abiria huyo wa milioni moja wa Fastjet, baada ya kupewa ofa ya kuchagua kusafiri kwenda katika sehemu yeyote tofauti inayokwenda nchini, alisema, “Napenda kusafiri kwenda Mwanza halafu nielekee Bukoba kuweza kuwasalimia wakwe zangu.”
Shirika hilo linatoa safari kati ya Dar es Salaam na mji huo wa ‘Rock City’ mara tatu kwa siku na kwa sasa ndio safari inayojaza abiria kwa wingi kupitia sehemu zozote zingine.
Bw. Kibati baada ya kumzawadia Bi. Makazi na tiketi mbili alisema, “Fastjet Tanzania inayofuraha kusafirisha abiria wake wa milioni moja ndani ya miezi 25 tangu kuanza kwa safari zetu nchini. Hii imefanikishwa kutokana na abiria walio wazalendo kwetu na wafanyakazi walio weka jitihada ya dhati kabisa katika haya mafanikio.”
Tangu kuanzishwa kwa shirika hili nchini mwaka 2012, Fastjet imekuwa kwa kasi kama shirika la ndege la gharama nafuu ndani ya Afrika Mashariki huku idadi ya abiria ikizidi kuongezeka siku hadi siku.
“Tunafikia malengo yetu ya ukuaji kwa kuwapatia wetu unafuu wa bei za tiketi za kusafiria na nyongeza ya safari kwenda ruti tofuati tofauti nchini. Fastjet inayofuraha kubwa kusaidia kufungua anga za Afrika,” alieleza Kibati. Shirika hili la Kitanzania ilifanikisha hili kwa kufanya safari zake bila kuchelewa kwa asilimia 90 ndani ya mwaka 2014 kutokana na maelezo ya meneja huyo.
Bw. Kibati pia alielezea kwamba pamoja na kwamba Afrika ina idadi kubwa ya watu zaidi ya bilioni moja, bara hili lina asilimia tatu tu ya abiria wote wanaosafiri duniani. Akidhihirisha mchango wa Fastjet katika kutoa huduma ya safari za ndege kwa gharama nafuu kwenda sehemu tofauti tofauti, “Mwaka huu tunatarajia kuongeza huduma zetu kwa kushirikiana na wadau mabali mbali na taasisi zenye dira kama serikali ya Tanzania ambao ni wadau wakubwa sana na wenye uelewa wakuendeleza uunganishwaji wa miji tofauti tofauti kupitia anga barani Afrika.”
Toa Maoni Yako:
0 comments: