DSC_0312

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige (kushoto) akiwasili kuzindua rasmi duka la urembo la ZuRii House of Beauty linalomilikiwa na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina George Meru (kulia) ndani ya jengo la Dar Free Market jijini Dar es Salaam jana.

Na Mwandishi Wetu

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige amezindua rasmi rasmi duka jipya la vipodozi na vitu mbalimbali linalofahamika kwa jina la ZuRii lililopo katika jengo la Dar Free Market lililopo katika barabara ya Alli Hassan Mwinyi Jijini Dar es Salaam.

Akizindua duka hilo ambalo linamilikiwa na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina George, Magige alisema kwamba amevutiwa na namna Jestina alivyoweza kurudi na kuwekeza nyumbani hali ambayo imeweza kuzalisha ajira kwa watanzania na kuwa mfano wa kuigwa.

“Kabla ya yote nachukua fursa hii kumpongeza Jestina kwani ameonesha mfano wa umuhimu wa kujiajiri hasa kwa wanawake pia huu ni mfano wa kuigwa kwa wanadiaspora , wengine warudi na kuja kuwekeza nyumbani kwani fursa nyingi zipo hivyo waje wazitumie” alisema Magige.

Aidha alitoa rai kwa wanawake wengine hapa nchini ambao wanauwezo wa kuwa na mitaji ya kuanzisha biashara wajiajiri na kutoa ajira kwa wengine pia natoa wito kwa watanzania wengine waje katika duka la ZuRii kuja kutoa sapoti kwa Jestina, alisema Magige.

Wakati huohuo mmiliki wa duka hilo la ZuRii Jestina alisema kwamba yeye ameona fursa za kuwekeza nyumbani hivyo ameamua kuzitumia ipasavyo.

“Natoa wito kwa kwa wanadiaspora wenzangu ni kwamba wasiwe na tabia za kuja likizo nyumbani nakuinjoi tu fedha zao tu bali wajitahidi kuja kuwekeza kwani fursa zipo, kuanzisha duka hili ni ndoto yangu ya siku nyingi hivyo haya ni matokeo ya njozi yangu namshukuru Mungu kwa kutimiza ndoto hii”.
DSC_0317
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akikata utepe kuzindua rasmi duka la ZuRii House of Beauty linalomilikiwa na Mwana Diaspora ambaye pia ni Blogger Jestina George Meru (anayeshuhudia tukio hilo).
DSC_0262
Mmiliki wa duka la urembo la ZuRii House of Beauty na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina George Meru akitoa maelezo ya baadhi ya bidhaa zake za urembo ambazo ni original kutoka nchini Uingereza na Marekani kwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige.
DSC_0264
DSC_0303
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akiangalia bidhaa za urembo wa nywele ndani ya dula la ZuRii House of Beauty lililopo ndani ya jengo la Dar Free Market linalomilikiwa na Mwana Diaspora Jestina George Meru.
DSC_0296
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akikagua moja ya bidhaa za nywele ndani ya duka hilo.
DSC_0231
Mmiliki wa duka la urembo la ZuRii House of Beauty na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina George Meru akitoa ushauri na maelezo kwa baadhi ya wateja waliofika dukani kwake mara baada ya kuzinduliwa rasmi jana jijini Dar.
DSC_0170
Mwanalibeneke Khadija Khalili akiangalia baadhi ya bidhaa ndani ya duka ZuRii House of Beauty.
DSC_0193
Wateja wakiendelea kumiminika na kujichagulia bidhaa mbalimbali vikiwemo vibanio vya nywele vya wakubwa kwa watoto ndani ya duka ZuRii House of Beauty.
DSC_0228
DSC_0339
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) waliohudhuria uzinduzi huo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
DSC_0337
Mmiliki wa duka la urembo la ZuRii House of Beauty na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina George Meru akimpa mkono wa shukrani ya kubariki uzinduzi duka hilo Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige jana jijini Dar es Salaam.
Mmiliki wa Duka la Zurii, Jestina George katika akizungumza na wanahabari katika uzinduzi wa duka hilo leo.
Mmiliki wa Duka la Zurii, Jestina George katika akizungumza na wanahabari katika uzinduzi wa duka hilo jana.
Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii pamoja na waendeshaji wa mitandao hiyo wakiwa katika picha ya pamoja  katika uzinduzi wa duka hilo.
Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii pamoja na waendeshaji wa mitandao hiyo wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi wa duka hilo.
Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii pamoja na waendeshaji wa mitandao hiyo wakiwa katika picha ya pamoja  katika uzinduzi wa duka hilo.
Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii pamoja na waendeshaji wa mitandao hiyo wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi wa duka hilo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments:

Back To Top