BABA OYEEEEEE...
Msichana alikuwa amekaa na baba yake kibarazani, mara akamuona MVULANA ambaye friend wake akija, yule mvulana alipokaribia tu, yule msichana akamwambia:
MSICHANA: Umekuja kuchukua kile kitabu chako, kinachoitwa "DADDY IS AT HOME?" by Ngozi Okafor.
MVULANA: Hapana!, Nimekuja kuazima kitabu cha Maombi kama kinaitwa "WHERE SHOULD I WAIT FOR YOU?" by Ngũgĩ wa Thiong'o.
MSICHANA: Aaah! Icho sina ila ninacho kimoja kinaitwa "UNDER THE MANGO TREE" by Chimamanda Adichie.
MVULANA: Ooh! Vizuri, Basi usisahau kuja nacho kesho kitabu cha Okot p'Bitek kile kinachoitwa "CALL ME IN 5 MINUTES BEFORE" Utakapokuja shule.
MSICHANA: Usijali, tena nina kitabu kipya kinaitwa "I WON'T LET YOU DOWN" by Chinua Achebe.
Baba mtu akawatazama kisha akasema;
BABA: Vitabu vyote hivyo, mbona vingi sana, atavisoma vyote kweli
MSICHANA: Ndio Daddy, huyu mvulana hupo smart sana na ana akili atavisoma vyote hivyo!
BABA: Sawa! Usisahau kumpatie na kile ambacho nimekiweka pale juu ya meza, kinaitwa "I AM NOT STUPID, I UNDERSTOOD EVERYTHING YOU'VE BEEN SAYING" by Shakespeare!
Na kuna kingine nimekiweka juu ya kabati la vyombo, kinaitwa "IF YOU GET PREGNANT PREPARE TO GET MARRIED" by Wole Soyinka.
Toa Maoni Yako:
0 comments: