Chama cha Alliance for change and Transparency (Act-Tanzania) kinatarajia kufanya uchaguzi mkuu wa kwanza ndani ya chama wa kuchagua viongozi wapya wa kudumu januari 19 mwaka huu.
Uchaguzi huu unatokana na sheria ya usajili ya vyama inayotaka uchaguzi wa viongozi wa kudumu ndani ya chama ufanyike ndani ya mwaka mmoja ikiwa usajili wa kudumu wa chama umepatikana.
Akizungumza na waandishi wa habari Makamu mwenyekiti wa wa Chama hicho Upande wa Bara Shaban Mambo amešema kwamba hadi sasa wapo katika mgogoro mkubwa ndani ya chama kuhusiana na uchaguzi huo lakini wao kama wapenda demokrasia ya kweli wamejipanga kupambana na hilo kwa kufuata sheria ya usajili na wanaimani uchaguzi huo utafanyika kama ilivyopangwa na kamti kuu.
Aidha Makamu huyo amezungumzia suala zima la uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana ambapo amesema wao kama chama wamepokea kwa furaha matokeo hayo kwani wameweza kushinda wenyeviti wa mitaa,vitongoji pamoja na vijiji wapatao 71 na kwa upande wa wajumbe wameshinda 193.
Naye katibu Mkuu wa chama hicho Samson Mwingamba amefafanua na kukanusha suala la yeye kufukuzwa katika chama hicho kwa utovu wa nidhamu na mwenyekiti wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments: