Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo 
kushoto akizungumza jambo na waandishi wa habari hawapo pichani katika 
uzinduzi wa huduma mpya ya Chagua chochote Bayport italipia jana jijini 
Dar es Salaam. Kulia kwake ni Meneja Biashara, Thabit Mndeme.



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


 

TAASISI ya 
kifedha ya Bayport Financial Services, imezindua tena huduma mpya inayojulikana 
kama ‘Chagua chochote unachotaka Bayport italipia’, ikiwa na lengo la kuwapatia 
mikopo ya bidhaa mbalimbali wateja wao na Watanzania kwa ujumla.


Huduma hiyo ni mwendelezo wa ile 'Mikopo ya Bidhaa' ambapo watu wanakopeshwa bodaboda, sambamba na Bima ya Elimu iliyozinduliwa pia mapema mwaka jana kwa ajili ya kuleta urahisi katika mfumo wa maisha ya Watanzania wengi.


Akizungumza katika uzinduzi wa huduma hiyo mpya, Meneja Biashara wa Bayport Financial services, Thabit Mndeme, alisema huduma hiyo sasa itawapatia fursa wateja wao kukopeshwa magari, nyumba, vifaa vya ujenzi, pembejeo za kilimo, ada ya shule,  pikipiki, bajaj, tv, injini ya boti na nyinginezo kwa ajili ya kuwapatia mwangaza mzuri wa kimaisha na kiuchumi.




Alisema kuwa kuanzisha huduma hiyo mpya imetokana na ile ya mikopo ya bidhaa kufanya vizuri tangu ilipozinduliwa mwishoni mwa mwaka jana na kupatikana nchi nzima kwa kupitia matawi yaliyosambaa katika mikoa mbalimbali.

Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme kulia akizungumza jambo katika uzinduzi wa huduma mpya ya 'Chagua chochote Bayport italipia', ikiwa ni mwendelezo wa huduma ya mikopo ya bidhaa, ambapo wateja wa Bayport wanapata fursa ya kukopeshwa bidhaa mbalimbali, kama vile nyumba, magari, vifaa vya ujenzi na nyinginezo. (Picha zote na Mpiga Picha Wetu).



“Bayport ilifanya mazungumzo na wateja wake mbalimbali baada ya kuzindua huduma ya Mikopo ya Bidhaa na kuona mafanikio makubwa waliyopata, hivyo mwaka huu tumeona tufike mbali zaidi kwa kuangalia namna gani Watanzania wanaweza kukopeshwa bidhaa nyingi kwa ajili ya kukuza uchumi wao.


“Ni rahisi mno kupewa mkopo wa chagua chochote unachotaka Bayport italipia kwasababu anachotakiwa kufanya mteja ni kuchagua bidhaa anayoitaka katika duka au msambazaji yoyote aliye karibu naye, kisha atapewa fomu ya malipo na kuipeleka kwenye tawi la Bayport lililo karibu yake ili apate mkopo aliyohitaji,” alisema Mndeme.


Alisema kuwa baada ya kuzinduliwa huduma hiyo ya Mikopo ya Bidhaa, wengi waliipenda na kunufaika nayo, hivyo aliwaomba wateja wao na Watanzania kwa ujumla kuendelea kuiunga mkono Bayport Financial Services kwa ajili ya kuwapatia maisha bora, maana ndiyo kusudio lao.


Naye Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kwamba taasisi yao inayojihusisha na mambo ya mikopo inatambua namna bora ya matokeo mbalimbali ya kuwaendeleza kiuchumi, hivyo huduma hizi ni mwendelezo wa juhudi za kukuza uchumi wa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni zilizoidhinishwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: