Mwili ukichukuliwa na Polisi baada ya kuvunjwa mlango wa chumba katika Guest House hiyo.
Askari polisi pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya mtaa kata ya Gongoni manispaa ya Tabora akiangalia mwili wa mwanaume mmoja ambaye ni Msusi katika moja ya Saloon za wanawake hapa manispaa ya Tabora inayofahamika kama HK.
Mwanaume huyo ambaye amefahamika kwa jina la Ramadhani amekutwa amefariki dunia akiwa chumbani katika nyumba ya kulala wageni inayofahamika kwa jina la SALAMA GUEST HOUSE ambapo ilidaiwa kuwa alikuwa ameishi katika nyumba hiyo kwa muda wa siku tatu kabla ya kufikwa na umauti.
Dada huyu inasemekana kuwa ndiye alikuwa mpenzi wake marehemu huyo Ramadhani.
Baadhi ya wananchi waliofika katika Guest house hiyo kushuhudia tukio hilo.
Picha na Habari kwa hisani ya Mdau Juma Kapipi. |
Toa Maoni Yako:
0 comments: