Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mh, Mwantumu Mahiza siku ya jumamosi wiki hii anatarajia kuongoza Bonanza la Wanavyuo linaloendea sehemu mbali mbali na ikiwa ni sehemu ya tatu kwa kanda ya kaskazini inayoendelea lwemye viwanja mbali mbali .

Bonanza hilo ambalo ni kwa ajili ya kupata timu zitakazoshiriki michuano ya NACTE linatarajiwa kuwa gumzo kwa mkoa wa Pwani kutokana na mfumo wake uliobuniwa kiufundi na waandaaji ambapo timu mbali mbali za Viongozi wa Serikali na zile za mkoa hupata fulsa ya kushiriki pamoja kwa kufanya michezo ya soka, kikapu,netball pamoja na Voleyball.

Akizungumzia bonanza la jumamosi Mratibu wa Michezo Vyuoni, Mpalule Shaaban alisema kuwa Mh, Mwantumu anatarajia kufanya Uzinduzi wa Michezo hiyo kwa Mkoa wa Pwani kutokana na kwamba sasa Michezo hiyo itafanyika kila mwaka Sehemu mbali mbali za Tanzania.

"Ni heshima ya pekee ambayo Serikali imetoa kwa Vijana wetu wa vyuo vya elimu ya kati kushiriki michezo, kumbuka kwamba michezo hii aijawahi kuwepo tangu NACTE imeanzishwa hivyo hii ni fulsa ya pekee tuliyonayo katika kuhakikisha kwamba tunahamasisha michezo hii wakati wote ili vijana wanaojiunga na Vyuo vya Elimu ya Ufundi, Veta, na wale wa ngazi ya Diploma kushiriki michezo vyuoni"alisema Mpalule.

Sehemu ya pili imefanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya ustawi wa jamii kijitonyama tarehe 29/11/2014, ambako Vyuo mbalimbali vya NACTE mkoa wa Dar es Salaam, vilicheza katika michezo ya soka, Basketball, Voleyball na netball,katika kutafuta timu zitakazoshiriki ligi ya NACTE Tanzania katika msimu wa 2014/2015.

sehemu ya kwanza Ilizinduliwa kwenye chuo cha DIT tarehe 22/11/2014 mwezi huu na kusisimua wengi katika Michuano lutokana na kuwa na mfumo wa mtoano kuwa kivutio kwa Wachezaji na Mashabiki ambao wengi wao ni wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali wanaofika kushuhudia michuano hiyo inayoendeshwa kwa ubunifu wa hali ya juu.

Vyuo vilivyokwisha cheza ni Institute of Adult Education, Institute of Social Work (ISW) - DSM, Lugalo Military Medical School - Dsm, St. Joseph College (University), Dar es salaam City College (DACICO, Dar-es-Salaam School of Journalism (DSJ) - DSM, National Institute of Transport (NIT) - DSM, Bandari College - DSM,huku timu mwalikwa ikiwa ni Timu ya wafanyakazi wa PPF Dsm.

Vyuo vingine ambavyo tayari vimemaliza michezo yao ya awali ni pamoja na IFM ,DIT, CBE, Muhimbili,TRA, Mlimani Profesianal,na Royal College, waliokuwa kundi la kwanza lililofanyika viwanja vya chuo cha DIT akiba Posta.

Aidha vyuo vyote vinavyohusika na michezo ya wiki hii zimetakiwa kuwahi Viwanjani ili kukamilisha taratibu za ukaguzi kabla ya michuano hiyo ya mtoano kuanza na ikumbukwe kwamba michuano hiyo inaendeshwa kwa mfumo wa Bonanza na inafanyika kila siku za jumamosi kutokana na wanafunzi kuwa masomoni katika siku za kawaida.

Kila mwaka michuano hii itakuwa ikifanyika kwa kushirikisha vyuo mbali mbali vya elimu ya kati hapa nchini Tanzania na vilivyopata usajili wa kudumu wa NACTE ambapo Kanda mbali mbali za Tanzania kupitia vyuo vyao vitashindana katika michezo mbali mbali kwa wavulana na wasichana ni vyuo 32 tu vitakavyokuwa vikishiriki baada ya kufanya mchujo wa awali kwa njia ya Bonanza na Timu mbili za juu kila BONANZA ndizo zitakazokuwa zikiingia katika idadi ya vyuo 32 vya NACTE ITER COLLEGE DAR ES SALAAM.

Ukiachilia mbali michezo hiyo, michezo mingine itakayokuwa ikifanyika kati ya wanafunzi na wanafunzi ni DEBATE, Marathon, Modoling, Mashindano ya Vipaji kwa viongozi wanaosimamia serikali za wanafunzi kwa nafasi za Rais na Makamu, Waziri Mkuu, Mawaziri wa Michezo,Fedha, na Spika , watakaokuwa wakichuana katika kujielezea, kujibu maswali, na kuelezea Mada katika nafasi zao na changamoto wanazokabiliana nazo na washindi watakuwa wakipata tuzo mbali mbali kulingana na ushindi wa kila mmoja.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: