Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog, Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Tanzania Mizengo Peter Pinda amesema ipo haja kwa serikali kushirikisha sekta binafsi katika kutatua changamoto mbalimbali zinazo ikumba sekta ya afya nchini ili nchi ifanye vizuri zaidi katika upande huo.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam mara baada ya kufungua mkutano uliowahusisha wadau wa afya nchini lengo likiwa kujadili namna ya kuiendeleza na kukuza sekta hiyo katika Nyanja mbalimbali.
Pinda amesema kwamba ipo haja ya kuwapa nafasi wawekezaji kuwekeza katika vyuo vya elimu ya juu vya sekta ya afya iliwaweze kutoa wataalamu wengi zaidi na kuondoa majukumu mengine kwa serikali.
Aidha Mheshimiwa Pinda amesema kwamba wao kama serikali wejipanga vizuri katika suala zima la Ugonjwa wa Ebola nchini ambapo wamewasihi wa viongozi wote wa halmashauri kuendelea kutoa elimu kuhusiana na ugonjwa huo kwani bado ni tishio.
Aidha Katibu Mkuu wa wizara ya Afya Dkt Donald mbando amesema kwamba mkutano huo unalengo la kutoka na mpango mkakati utao tekelezeka kwa kufuata mpango wa matokeo makubwa sasa ambapo wataanza kusambaza wafanyakazi upya wa afya ili kila mkoa uweze kuwa sawa na mwingine.
Mkutano huo utajadili mambo mbalimbali ambapo yakitekelezwa yataweza kuikuza sekta ya afya na kuifanya izidi kwenda mbele
Toa Maoni Yako:
0 comments: