Katibu wa Itikadi na Uenezi, Ndugu Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo ya makao makuu Lumumba, leo asubuhi.
---
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahaman Kinana kesho November 15, 2014 anatarajia kuanza Ziara katika Mikoa ya Kusini (Lindi na Mtwara). Ziara hiyo ya Katibu Mkuu inategemea kuanza kesho katika wilaya ya Kilwa iliyopo Lindi na Kisha kuendelea katika wilaya zingine kwa takribani siku kumi na sita za kutembelea majimbo, kata, matawi na mashina ya Chama Cha Mapinduzi.
Ziara hii ya Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahaman Kinana ni muendelezo wa Ziara za Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi ambazo zimekuwa zikiendelea kote nchini tangu Sekretarieti hiyo ilipoteuliwa mwanzoni 2012.
Malengo ya ziara hii ni kukagua uimara wa Chama katika mikoa hiyo pamoja na kujenga na kuhimiza Uhai wa Chama katika kanda ya kusini ambayo kwa muda wote imeendelea kuwa ngome muhimu kwa Ushindi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Lakini pia ziara hii inalenga Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2010 - 2015 ambayo imeendelea kutekelezwa kwa mafanikio na Serikali katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Tunawaomba wananchi wa Mikoa ya Kusini kuwa tayari kujitokeza kwa wingi katika Mikutano ya hadhara iliyoandaliwa na kusema kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili ili ziweze kufanyiwa kazi na kutekelezwa mara moja.
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu ataongozana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi, ndugu Nape Nnauye.
UMOJA NI USHINDI.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
Toa Maoni Yako:
0 comments: