Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
WATANZANIA leo tunaadhimisha kumbukumbu ya miaka 15 tangu kufariki kwa muasisi na Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mwalimu Nyerere alifariki dunia Oktoba 14, 1999 akiwa nchini Uingereza alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na maradhi ya kansa ya damu.
---
Wosia wa Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere uliomo kwenye hotuba zake;
“Katika nchi kama yetu, ambayo Waafrika ni maskini na wageni ni matajiri, kuna uwezekano mkubwa kwamba Mwafrika akiruhusiwa kuiuza ardhi, katika miaka themanini au miaka ijayo, ardhi yote ya Tanganyika itamilikiwa na matajiri wageni, na wenyeji watakuwa watwana. Lakini hata kama wageni wasingekuwa matajiri, litaibuka tabaka la Watanganyika matajiri wajanja. Tukiruhusu ardhi iuzwe kama kanzu, katika muda mchache, kutakuwa na kundi dogo la Waafrika wakiwa na ardhi na walio wengi watakuwa watwana.” Na. Mwl. J.K. Nyerere ( 1958)
"Siku inakuja ambapo watu watachagua kifo kuliko kubaki na fedheha. Ole wao watakaoishuhudia siku hiyo. Na ole wao zaidi wale watakaosababisha siku hiyo ifike. Nasali nikitumaini nisiwe sababu ya siku hiyo kutokea. "
Na. Mwl. J.K. Nyerere ( 1966)
"Mwanadamu anakuwa ameendelea pale anapojitosheleza mwenyewe kwa mahitaji ya msingi. Lakini pale anapotoshelezwa na mahitaji hayo na mtu mwingine huyo hatusemi ameendelea bali ameendekezwa. Kuendelea na kuendelezwa vyote hutosheleza mahitaji ya mtu. Lakini kimojawapo humwacha mtu akiwa mtumwa. Maendeleo hata yakija polepole ni muhimu kwa sababu ya uhuru wa kudumu"
Na. Mwl. J.K. Nyerere ( 1973).
"Kupima maendeleo kwa kuhesabu GDP (pato la ndani la taifa) ni kupima vitu badala ya kupima shibe. Maendeleo ya kweli utayapima kwa kuhesabu kama watu wamekula chakula bora na kushiba, wametibiwa na kupona, na wamesoma na kuelimika. GDP ni kipimo cha maendeleo cha wanasiasa na wafanyabiashara ili wapate takwimu za kuwavutia wahisani na wawekezaji. Lakini maendeleo ya kweli hayako huko"
Na. Mwl. J.K. Nyerere ( March 1973, Kharthoom Sudan)
"Hatuwezi kulaani mauaji halafu tukabaki tumewakumbatia wauaji. Kama watu wanahujumu ustawi wetu tuwaambie hapa. Wakitusikia wakaacha tubaki nao. Wakiwa wakaidi tuwatenge na kuwatangaza kuwa ni adui"
Na. Mwl. J.K. Nyerere ( February 1994 Arusha)
“Watanzania wanataka mabadiliko; wakiyakosa ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM”
Mwl J.K Nyerere (1995 Dodoma).
“Habari ni habari utasikia fulani kampiga mkewe hiyo si habari, lakini Nyerere kampiga mkewe hiyo ni habari itaandikwa kweli kweli”. Mwl JK Nyerere.
“Kiongozi atakayepokea rushwa, tukimkamata tutamfunga miaka miwili na atapigwa viboko 24; 12 akiingia na kumi na mbili akitoka, aende akamwonyeshe mkewe. Mwl JK Nyerere.
“Nang’atuka, lakini bado nasisitiza kuwa, bila CCM imara nchi yetu itayumba” 1990s. . Mwl JK Nyerere.
“Serikali ikitawaliwa na rushwa haiwezi kukusanya kodi, itabakia kukimbizana na watu wadogo wadogo tu”. Mwl JK Nyerere.
“Serikali ya Tanzania haina Dini”. Mwl JK Nyerere.
” Mara hii tu mmetajirika kiasi hicho? Kama mmeweza kutajirika kiasi hicho katika muda mfupi, fanyeni basi wote tutajirike, kwa nini mtajirike peke yenu?!”. Mwl JK Nyerere.
“Kwa mtu mwaminifu kabisa, Ikulu ni mzigo, si mahali pa kukimbilia hata kidogo”. Mwl JK Nyerere.
Toa Maoni Yako:
0 comments: