Dear Mama,
Zimepita siku, wiki, miezi sasa umetimiza mwaka. Tunashindwa kuamini kwamba haupo pamoja nasi lakini hata tukizunguka nyumba hatukuoni tangu ile siku 14/10/2013 pale Mungu alipokupenda zaidi.
Mama tunakosa upendo wako, ushauri wako na umakini wako katika maisha.
Tunapenda kuwashukuru majirani zetu wote wote pale Kawe Mzimuni, Jumuiya na Mt. Bonaventura ya Kawe Mzimuni, Mtaa wa Barazani na Parokia ya Kawe kwa msaada mkubwa mlipotupatia mpaka kufanikisha mazishi ya mama yetu mpendwa. Pia tunawashukuru Wanachana wa Legio Maria tangu Parokia ya Kawe mpaka Jimbo kwa kuwa pamoja nasi katika shughuli nzima ya mazishi ya mama yetu.
Hatuwezi kusahau kumshukuru Dr. Pascal wa Usambara Arafa Dispensary ya Kawe kwani uhai wa mama yetu mpaka kufika hiyo tarehe 14.10.2014 ulikuwa mikononi mwao kwa msaada mkubwa na dawa na ushauri. Siyo rahisi kumshuru mtu mmoja mmoja bali tunatoa shukrani nyingi sana kwa majirani zetu wote walitoa msaada wao wa hali na mali. Wafanyakazi wa Engen Petroleum si wa kuwahasahau katika hili kwani michango yao katika kufanikisha mazishi ya mama yetu mpendwa yalikuwa msaada mkubwa bila kusahau Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Misa za Kumuombea Marehemu zinafanyika katika Kanisa na Mt. Michael Parokia ya Kawe kuanzia Jumatatu 13/10/2014 zitahitimishwa Jumapili 19/10/2014.
Mama tunakuombea ili upumzike kwa amani ni sisi wanao:
Cecilia Mahundi, Joseph Mbunda, Veronica Mbunda, Rosazalia
Mbunda na wajukuu zako wote.
Mungu ailaze roho yako mahala peponi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: