Mafunzo ya elimu ya ujasiriamali kwa washiriki wa shindano la Mashujaa wa Kesho yamekamilika wiki hii. Mafunzo hayo yanayoratibiwa na kampuni ya Statoil Tanzania ni sehemu ya shindano la Mashujaa wa Kesho lililoandaliwa kwa ajili ya kukuza ubunifu wa kibiashara kwa vijana wa Mtwara.

Akibainisha aina ya mafunzo ya ujasiriamali waliyopata vijana hao, Erick Mchome, Afisa Uhusiano wa Statoil-Tanzania amesema kuwa vijana wamefundishwa namna ya kuandika wazo au mpango wa biashara kwani baada ya mafunzo hayo, kila mshiriki atatakiwa kuandika wazo lake la biashara.

Elimu nyingine iliyotolewa katika mafunzo hayo ni elimu ya ujasiri. Lengo la mafunzo ya ujasiri ni kuwajengea washiriki uwezo wa kuwasilisha mawazo yao ya biashara mbele ya majaji wakati wa kutafuta washindi watano.

Elimu hiyo itawasaidia vijana hao hata baada ya shindano kukamilika kwani mjasiriamali anahitaji kujiamini na kuwa na uwezo wa kusimama mbele ya watu na kujieleza kwa ufasaha ili aweze kufanikiwa katika biashara yake.

Sehemu nyingine ya mafunzo hayo ilihusu elimu ya ujasiriamali. Mafunzo ya ujasiriamali yamelenga kuwajenga vijana hao katika msingi wa kijasiriamali na hivyo kuwa na vijana watakaokuwa wajasiriamali wakubwa siku zijazo katika jamii ya Mtwara. Vijana wamefundishwa namna ya kuanzisha biashara,

kukuza biashara, kujua mapato na matumizi katika biashara, kuwa na nidhamu katika biashara, na kukuza biashara zao na kuwa za kimataifa.

Kwa upande wao, vijana walioshiriki mafunzo hayo wamesema kuwa elimu waliyoipata imewapa mwanga mkubwa kuhusu biashara na imewapa ujasiri wa kuwa wajasiriamali na kuachana na dhana ya kutegemea kuajiriwa.

“Nawashukuru Statoil-Tanzania pamoja na wasimamizi wa mafunzo haya kwani elimu tuliyopata hapa ni msingi mkubwa utakaotuwezesha kuwa wajasiriamali, kufanya biashara zetu wenyewe na kuachana na kutegemea ajira kutoka serikalini kwani tatizo la uhaba wa ajira linazidi kuwa kubwa kadri siku zinavyozidi kwenda”, Alisema Ally Seleman mshiriki wa shindano la Mashujaa wa kesho.

Mafunzo ya elimu ya biashara na ujasiriamli yalianza tarehe 27 Oktoba 2014 na kufikia tamati yake tarehe 30 Oktoba. Mara baada ya mafunzo hayo

kukamilika, vijana wamepewa siku 12 za kuandika mawazo yao ya biashara na kuyarejesha siku ya Jumatano tTrehe 12 Novemba ili majaji wayapitie na kuchagua kwa washindi watano ambapo mshindi wa kwanza atajipatia dola 5,000 na washinde wengine wanne kupata dola 1,000 kila mmoja ifikapo Desemba 4, 2014.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: