Msanii chipukizi wa kijiwe cha Matofali jijini Morogoro ajulikanaye kwa jina la Jibwa Kali akionyesha umahiri wake wa kuimba wakati Airtel ilipotembelea vijiwe mbalimbali mkonia Morogoro na kuzindua mashindano ya Airtel Trace Mkoani humo.
Meneja Uhusiano wa Airte Bwana Jackson Mmbando akiongea na wasanii chipukizi wa Kijiwe cha Matofali mkoani Morogoro wakati Airtel ilipotembelea vijiwe mbalimbali mkonia Morogoro na kuzindua mashindano ya Airtel Trace Mkoani humo

*Wasanii chipukizi kutoka morogoro watembelewa katika vijiwe vyao na kujiunga na mashindano ya Airtel Trace

Kampuni ya simu za mkoni ya Airtel imeendelea kuwafikishia wateja wake na wapenzi wa muziki katika mikoa mbalimbali na kuwaunganisha katika mashindano ya kutafuta mwamamuziki chipukizi ya Airtel Trace yaliyozinduliwa rasmi nchini mwanoni mwa mwezi octoba. Airtel imetembelea Mkoa wa Morogoro na kuzindua rasmi huduma ya Airtel Trace music star katika vijiwe mbalimbali mkoani hapo

Akizungumza na wasanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya katika vijiwe mbalimbali mjini Morogoro, Meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando amesema huduma hiyo inamuwezesha mtu yeyote mwenye kipaji cha kuimba kujiunga na kushiriki kwa kupitia simu ya mkononi kwa kupiga namba 0901002233 kisha kurekodi wimbo wake na kuutuma.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: