Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
TAMASHA kubwa la umataduni linalojulikana kama 'Handeni Kwetu' limepangwa kufanyika Desemba 13 mwaka huu, katika Uwanja wa Azimio, wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Mratibu Mkuu wa Tamasha la Handeni Kwetu, Kambi Mbwana, akizungumza jambo katika tamasha la mwaka lililofanyika Desemba 14. Mwaka huu tamasha hilo litafanyika Desemba 13, Siku ya Jumamosi, katika Uwanja wa Azimio, wilayani Handeni, mkoani Tanga. Picha na Maktaba Yetu.
Wasanii wa kundi la ngoma za asili la Mgambo JKT, wilayani Handeni, mkoani Tanga, wakitoa burudani katika tamasha hilo mwaka jana. Mwaka huu litafanyika Desemba 13, Siku ya Jumamosi, katika Uwanja wa Azimio, wilayani Handeni, mkoani Tanga. Picha na Maktaba Yetu.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu (katikati), akifurahia katika tamasha hilo mwaka jana lililofanyika Desemba 14. Mwaka huu litafanyika Desemba 13, Siku ya Jumamosi, katika Uwanja wa Azimio, wilayani Handeni, mkoani Tanga. Kulia kwake ni Afisa Utawala wa wilaya ya Handeni, Upendo Magashi. Picha na Maktaba Yetu.
Katika tamasha hilo linalofanyika kwa mara pili, burudani mbalimbali za ngoma za asili zinatarajiwa kuonekana jukwaani, ambapo pia vikundi kutoka nje ya Handeni, mkoani Tanga navyo vitaalikwa kwa ajili ya kwenda kutoa burudani wilayani humo.
Akizungumzia hilo, jijini Dar es Salaam, Mratibu Mkuu wa tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema kuwa maandalizi ya tamasha hilo yanawekwa ili kuliweka katika kilele cha ubora na kuchangia maendeleo ya sanaa na uchumi kwa ujumla.
Alisema kuwa mwaka jana tamasha hilo lilianza kwa mafanikio makubwa, ambapo wageni mbalimbali walifika wilayani humo, jambo lililochangia pia kuitangaza Handeni na mkoa mzima wa Tanga.
“Mwaka huu tumeweka mikakati kabambe ya kuhakikisha kuwa tamasha letu linaendelea kukua kwa kasi baada ya kuanzishwa kwa mafanikio makubwa mwaka jana.
“Naamini kuwa haya ni matunda ya kushirikiana kwa pamoja na wadau wote, ikiwamo serikali kwa kupitia ofisi zote za wilaya ya Handeni, hivyo watu wajiandae mambo mazuri na makubwa kutoka kwenye tamasha hili,” alisema Mbwana.
Tamasha la utamaduni la Handeni, linalojulikana kama Handeni Kwetu, ni miongoni mwa matamasha yenye mchango mkubwa, ambapo kwa mwaka jana Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ndio waliokuwa wadhamini wakuu na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuliweka katika mguso wa aina yake.
Toa Maoni Yako:
0 comments: