Ni miezi minne sasa toka nimpoteze mama yangu mzazi, kipenzi changu, rafiki yangu wa kweli, mfariji wangu, mshauri wangu, nguzo yangu... kifo chake kimenipa mafunzo mengi mno kama mapenzi yake ya kipekee kwangu, kujitoa kwa kila hali kuhakikisha sipungukiwi chochote ktk maisha yangu na kama haitoshi nikagundua wamama wana siri kubwa sana za mapito ktk malezi ya watoto wao, kama kuna kitu nakihitaji zaidi maishani basi ningependa mama yangu arudi tena japo kwa muda flani ... nina mambo mengi mazuri nilipanga kumfanyia mamangu lakini ndo hivyo.
Pia nimejifunza wanadamu walivyo vigeugeu kuanzia ndugu, marafiki na jamaa. Namkumbuka mno na wakati mwingine siamini kama kweli hayuko nami, pengo lake halitokaa likazibika.UPENDO WA MAMA NI WA KIPEKEE, HAKUNA KAMA MAMA. Love your mum today as if tomorrow she will be going far away for a longtime...
Ni Mimi Rinee Belle.
Toa Maoni Yako:
0 comments: