Ben Pol akiwa Voice of Africa, Muheza Tanga akieleza namna alivyojiandaa
Malkia wa mipasho Khadija Kopa akihojiwa ndani ya Breeze FM Tanga
 Joh Makini na GNako wa kundi la Weusi katika interview
Rich Mavoko akiingia katika Tour Bus jijini Tanga

Na Mwandishi Wetu.

MFALME na Malkia wa Taarab, Mzee Yusuph na Khadija Kopa, ni miongoni mwa wasanii wanaotarajiwa kupamba show ya Kili Music Tour inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager itakayofanyika kesho katika Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.

Wawili hao ni miongoni mwa wasanii wenye kupendwa hasa katika mikoa ya ukanda wa Pwani na Tanga huku wao wakiahidi kumwaga burudani ya nguvu ikiwa ni ya mwisho kwa mikoani kabla ya kufungwa jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema jana kuwa, lengo la ziara hiyo yenye kauli mbiu ya ‘Kikwetu Kwetu’ ni kukuza muziki wa ndani na pia kuwapa burudani wapenzi wa muziki mikoani.

“Ziara hii ina lengo la kuwapeleka wasanii kwa wananchi na pia ina lengo la kukuza muziki wetu wa ndani ndio maana tulichagua kauli mbiu ya kikwetu kwetu yaani tunajivunia kilicho chetu,” alisema Kavishe.

Show ya Tanga itakayofanyika Uwanja wa Mkwakwani, inatarajiwa kuanza saa kumi jioni hadi usiku sana. Kavishe alisema kiingilio katika tamasha hilo ni tsh 3,000 na kila anayeingia atapata bia moja ya Kilimanjaro Premium Lager, lakini awe ametimiza au zaidi ya umri wa miaka 18.

Mbali ya Mzee Yusuph na Khadija Kopa, wengine watakapamba shoo hiyo ni Prof. J, Rich Mavoko, Ben Pol, Weusi na Ommy Dimpoz. Hii ni ziara inayoratibiwa na makampuni ya East Africa TV na radio, Executive Solutions, Aggrey and Clifford, Integrated Communications na Aim Group.

Ziara hiyo inatua Tanga ikitokea Mkoani Kigoma kabla ya hitimisho la aina yake litakalofanyika Septemba 6, jijini Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: