4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akifunua jiwe la msingi wakati wa ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa huko Mkuzo wilayani Songea Mjini, mkoani Ruvuma jana. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw. David Misonge Shambwe na wa pili kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka, kulia ni Mama Salma Kikwete, Mke wa Rais.
5
Rais Jakaya Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mh. Saidi Mwambungu (kulia), Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw. David Shambwe wakikata utepe kwa pamoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi huo.
6
Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw David Shambwe akitoa taarifa za mradi wa huo wa gharama nafuu wa Mkuzo kwa Rais Dr. Jakaya Kikwete.
8
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii Cha Shirika la Nyumba la Taifa (National Housing) Susan Omari akitoa maelezo kwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuhusu mashine za kutengeneza matofali aina ya Hydraform ambazo zitagawanywa kwenye wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma ili kuwezesha vikundi vilivyoanzishwa vya ujenzi vya vijana kuendelea na mafunzo . Anayezishuhudia Mashine hizo ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna kajumulo Tibaijuka.
9
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Saidi Mwambungu wakizishuhudia mashine za kufyatulia matofali aina ya Hydraform ambazo zitagawanywa kwenye wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma ili kuwezesha vikundi vilivyoanzishwa vya ujenzi vya vijana kuendelea na mafunzo .
10
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka akizungumza katika hafla hiyo jana, kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Pombe Magufuli, wabunge na viongozi mbalimbali wa mkoa huo walioshuhudia tukio hilo.
11
Rais Dr. Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, ambapo aliziagiza halmashauri za miji kuzipa maeneo taasisi mbalimbali za umma zinazojishughulisha na masuala ya uendelezaji miji ili waweze kupanga miji vizuri na kuboresha madhari.
12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wananchi waliofika kushuhudia
13
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakiwasalimia wananchi waliofika kushuhudia
14
Wananchi waliofika kushuhudia tukio la uzinduzi wakiwa wamejipanga kando ya barabara.
15
Msafara wa Rais ukiondoka jana katika eneo la tukio baada ya kumaliza ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa huko Mkuzo wilayani Songea Mjini, mkoani Ruvuma.
16
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mojawapo ya nyumba iliyokuwa ya mfano wakati wa ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa huko Mkuzo wilayani Songea Mjini, mkoani Ruvuma.
1
Kikundi cha ngoma na burudani kikiburudisha hadhira iliyofika eneo hilo la Mkuzo kabla ya Rais kufika.
---
Rais Kikwete amerejea kauli yake aliyoitoa Kasera, Mkinga Tanga kwamba Halmashauri zizipatie taasisi zingine zinazojishughulisha na uendelezaji miliki kama NSSF, PPF, GEPF, PSPF, LAPF na kadhalika maeneo kwa masharti ili ziweze kujenga.

Rais Kikwete aliambiwa kuwa katika eneo hilo la Mkuzo, shirika hilo limejenga kiasi cha nyumba 18 za kuuza na zimejengwa kwa gharama ya sh. milioni 676.

Rais Kikwete pia ameambiwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Bw. David Misonge Shambwe kuwa nyumba hizo zimejengwa katika kutekeleza kaulimbiu ya NHC ya "Nyumba yangu, Maisha yangu" ambayo mpaka sasa inatekelezwa katika mikoa 14. Ujenzi wa nyumba hizo ulianza Januari mwaka jana na unakamilika mwezi ujao, Agosti, 2014.

Nyumba hizo, ameambiwa Rais Kikwete, kuwa zitauzwa kwa gharama ya kati ya sh. milioni 33 na 44 bila kodi ya VAT lakini ambayo inaongezeka na kuwa kati ya milioni 44 na 52 kwa kutegemea ukubwa wa nyumba - kuanzia ya vyumba viwili hadi nyumba vitatu. Rais Kikwete anaendelea na ziara yake mkoani humo.

Mkuzo Housing Estate ni mradi wa nyumba 18 zilizopangwa kwa kuzingatia vigezo vya miji ya kisasa yenye huduma za msingi zikiwemo Zahanati , shule ya Chekechea , maduka , sehemu za shughuli mbalimbali za jumuiya, barabara pana inayotoa fursa kwa watembea kwa miguu na baiskeli kuwa huru vile vile imezingatia nafasi za miundombinu kama vile mitaro na umeme.
Kila nyumba inajitegemea ikiwa na eneo kubwa kwaajili ya matumizi binafsi ya wakazi pamoja na eneo la maegesho ya magari hadi matatu.

Mkuzo Housing estate ina nyumba za aina mbili, nyumba za vyumba vitatuna nyumba za vyumba viwili . Nyumba za vyumba vitatu zin aukubwa wa mita za mraba 85 kwa zile zenye jiko la nje na mita 70 zenye jiko la ndani. Huku nyumba ya vyumba viwili ikiwa na mita za mraba 56. Zinauzwa kati ya Sh 33 milioni bila VAT na 44 milioni.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: