*Yakataza wafanyakazi kutumia simu wanapoendesha magari
Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imezindua kampeni maalum ya kuhamasisha wafanyakazi wake kuhakikisha uendeshaji wa magari na vyombo vingine vya moto unaozingatia usalama ili kulinda afya na usalama wao wawapo barabarani.
Vodacom ambao ni washindi wa tuzo ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi inayotambuliwa na Mamlaka ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) imezindua kampeni hiyo ikiwa ni mwendelezo wa jitihada mbalimbali inazozichukua katika kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wake wakati wote wanapokuwa kazini.
Kampeni iliyozinduliwa ya “Wait to Send Campaign” inawataka wafanyakazi wa Vodacom wanaotumia magari ya kampauni na wasiotumia kutotumia simu ya mkononi kutuma ama kusoma ujumbe mfupi wa maandishi ili kujiweka katika mazingira salama ya kujikinga na ajali wawapo barabarani.
“Tunayofuraha kubwa sana leo kuona tunapiga hatua nyingine moja ya ziada katika kulinda afya na usalama wa wafanyakazi wetu wakati wote. Hili ni jukumu letu tunalolipa kipaumbele cha hali ya juu katika uendeshaji wa shughuli zetu.”Alisema Mkuu wa Idara ya Usalama, Afya na Mazingira wa Vodacom Tanzania Karen Lwakatare.
“Kila mfanyakazi wetu lazima awe salama na tunapotambua uendeshaji wa majukumu yetu ambao matumizi ya magari na vyombo vingine vya usafiri ni sehemu ya kazi zetu na amsiha yetu ni lazima tukumbushane njia bora za uendeshaji ulio salama kwa faida yao na kwa kampuni pia.”Alisema Lwakatare
Lwakatare amesema ingawa hakuna ajali nyingi zinazowahusisha wafanyakazi wakiwemo wakandarasi wake lakini jambo hilo haliwezi kuifanya Vodacom kujisahau kwani lengo ni kuhakikisha hata hizo chache zinazojitokeza zinadhibitiwa na kuepukwa.
Amesema matumizi ya simu za mkononi kwa madereva ni moja ya visababishi vya ajali na hasa kutumia simu ya mkononi kutuma au kusoma ujumbe mfupi wa maadishi na kwamba wanataka kila mfanyakaizi atambue hilo na kujikinga dhidi ya janga analoweza kulipata kwa kutumia simu yake anapoendesha gari.
Amesema Vodacom inaangalia namna gani wanaweza kushirikiana na Jeshi la Polisi na wadau wengine kuendesha kuihusiha jamii nzima na kampeni hiyo ili kupunguza ajali za barabarani zinazochangiwa na matumizi ya simu za mkononi.
“Unaweza kuona kama ni kitu cha kushangaza kuwa sisi ndio watoa huduma za simu za mkononi halafu tunakataza matumizi ya simu hizo kwa madereva wawapo barabarani. Kwetu sisi maisha ya mteja wetu na mfanyakazi wetu ni yenye thamani kubwa zaidi kuliko jambo lolote.”
Vodacom Tanzania ni miongoni mwa makampuni yaliyowekeza vya kutosha katika kuhakikisha afya na usalama wa wafanyakazi wake mahala pa kazi huku kila mfanyakazi akitakiwa kutii amri kuu za usalama na afya wakati wote bila kukosa kwa kisingizio chochote.
Toa Maoni Yako:
0 comments: