Gari likiwa linarudi nyuma lilipotokea baada ya kuona kuna moshi mkubwa mbele yao.
 Mashuhuda wakiwa wameanza kuelekea eneo la tukio
 Moto ukiwa unaanza kupamba moto, waya wa umeme unao onekana unashuka chini ndio umesababisha moto huo.
 Duka la nguo likiwa linapamba moto na maduka mengine yakiwa yameanza kupamba moto pamoja na nyumba ambayo ilikuwa imeungana na duka.
 Mmoja ya vijana akiwa anaanza kuokoa vitu vyake jirani na maduka yaliyokuwa yakiungua.
 Moto ukiwa unazidi
 Mamia ya watu wakiwa wamefika kushuhudia  tutuki la Moto
 Maduka mengine yakiwa yameanza kushika moto kwa kasi
 Baadhi ya vyombo na vifaa vya duka la kushonea nguo vikiwa vimeokolewa
 Mashuhuda wakiwa wanaongezeka.
Vijana wasamalia wema wakiwa wameacha kazi zao za kutengeneza magari, kufyatua matofari na mambo mengine wakiwa wanafanya kazi ya kuanza kuuzima moto.
 Vijana wakiwa wameanza kufanya kazi ya kuzima moto baada ya Kikosi cha zima moto kuendelea kuchelewa kufika
Maduka yakizidi kwisha kwa kuteketea kwa moto, Huku wananchi wakipata tukio moja kwa moja
 Baadhi ya Vijana wasamalia mwema wakiwa wanaondoa mabati ili kuzuia moto usiendelee kuwaka zaidi
Sehemu ya nyaya za umeme uliosababisha moto huo.
 Vijana wakiendelea kufanya kazi ya kuendelea kuzima moto kwa ushirikiano.
 Baadhi ya Mashuhuda wakimwagiwa maji kupisha njia ya waokoaji waliojitolea kuzima moto kupita.
 Kikosi cha zima moto wakiwa wakiwa wanawasili eneo la tukio, huku wananchi wakiwazuia wasifanye kazi kwa kuwa kazi wamekuta imeisha
 Kikosi cha zima moto wakiwa wameanza shuguli ya kumalizia kuzima moto
Maji ya kuwasha yakiwa yamefunguliwa ili kuwatawanya watu wakae mbele kupisha kazi ya kuzima moto na uharifu.
 Kikosi maalum cha kuzuia vurugu cha Jeshi la Polisi (FFU) wakiwa  wamefika eneo la  tukio kwa ajili ya kulinda usalama
 TANESCO wakiwa wamefika eneo la tukio
 Watu wakiwa wanazidi kuzuiliwa kupisha kazi ya uokoaji.
 Kikosi Maalum cha kuzuia vurugu kutoka Jeshi la Polisi FFU wakiwa wanaongezeka kuongeza kuvu ya kuimarisha ulinzi
 Kazi ya uokoaji ukiwa unaishia
 Kikosi maalum cha zima moto wakiwa wanamalizia kazi ya kuzima moto kidogo uliobakia
 Kila mtu anajitahidi kupata tukio
 Kazi ikiwa inaelekea kumalizika
 Baadhi ya mabaki uya mabati.
 Hivi ndivyo maduka yalivyobakia pamoja na nyumba iliyo ungua
 Mabaki ya vitu katika duka la vitambaa ya nguo na ushonaji.
 Wananchi wa mwananyamala wakiwa wanasikika wakisema "Wamekuja zima moshi... wamekuja zima moshi..."
 Kazi ikiwa imeisha hizi ndizo ndoo ambazo zilisaidia kwa kiasi kikubwa kuzima moto pamoja na baadhi ya vijana wachache walio saidia kuzima moto huo.

Habari na Picha kwa hisani ya Dar es Salaamu Yetu Blog. 

Moto mkubwa uliosababishwa na hitirafu ya umeme  umewaka eneo la Mwananyamala Jirani na Hospitali ya Mwananyamala na kusababisha kuungua kwa Maduka matatu pamoja na nyumba moja ambayo ilikuwa imeungana na duka moja wapo ambamo walikuwa wanauza vitambaa na kushona nguo.

Moto huo ulichukua zaidi ya masaa mawili ambapo wakazi wa eneo hilo ndio waliosaidia kwa kiasi kikubwa kuzima moto huo mpaka kuumaliza na baadae Kikosi cha kuzima moto kufika na kukuta moto ndio unaishia na kuendelea kumalizia kushirikiana na wananchi wengine kuzima moto huo.

Katika tukio la Moto huo hakuna mtu ambaye amedhuriwa ingawa katima maduka yote matatu walifanikiwa kuokoa baadhi ya vitu huku vilivyobakia kuteketea vibaya kwa moto huo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: