Mkurugenzi wa Tanzania House Of Talent (THT) Ruge Mutahaba akiongea katika halfa ya kumuaga msanii Linah jana Julai 16, 2014 kutoka kwao na kuelekea kampuni ya No Fake Zone (NFZ) ambao ndiyo wanaanza kumsimamia msanii huyo.
Mkurugenzi wa THT, Ruge Mutahaba akigawa cheti cha ustadi wa kazi wa Msanii Mwasiti ambaye ameitambulisha vyema taasisi yao tokea imenza.
Mtayarishaji wa Muziki Emma The Boy akiurahia jambo mara baada ya kupokea cheti chake cha ustadi bora wa kazi.
Mkurugenzi wa THT, Ruge Mutahaba akimpa zawadi ya cheti cha ustadi wa kazi wa Msanii Ditto ambaye ameitambulisha vyema taasisi yao tokea imenza.
Msanii Ditto akifurahia cheti chake cha ustadi wa kazi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya FNZ, Abby akiongea machache wakati wa hafla ya kukabidhiwa rasmi msanii Linah ili waweze kumsimamia kazi zake. Hafla hiyo ilifanyika jana Julai 16, 2014 ndani ya ofisi za THT jijini Dar es Salaam.
Msanii Linah akitoa shukrani zake kwa THT kwa jinsi walivyomlea tokea amejiunga mwaka 2009 na mpaka leo ameondoka. Pembeni ni Mkurugenzi wa Kampuni ya FNZ, Abby ambaye ndiye anayemchukua msanii huyo kumsimamia kazi zake. Hafla ya kumuaga Msanii huyo ilifanyika jana Julai 16, 2014 ndani ya ofisi za THT jijini Dar es Salaam
Msanii Linah akitoa zawadi kwa Mkurugenzi wa THT, Ruge Mutahaba katika hafla ya kumuaga Msanii huyo ilifanyika jana Julai 16, 2014 ndani ya ofisi za THT jijini Dar es Salaam
Msanii Linah akitoa zawadi kwa Mwalimu wake Nkya ambaye alikuwa msitari wa mbele kumuongoza mpaka leo amefanikiwa katika hafla ya kumuaga Msanii huyo ilifanyika jana Julai 16, 2014 ndani ya ofisi za THT jijini Dar es Salaam.
Msanii Linah akitoa zawadi kwa Rehema ambaye alikuwa msitari wa mbele kumshauri kwa mambao mbali mbali mpaka leo amefanikiwa katika hafla ya kumuaga Msanii huyo ilifanyika jana Julai 16, 2014 ndani ya ofisi za THT jijini Dar es Salaam.
Mtayarishaji wa Muziki na Msanii Nash Designer ambaye ndiye mtunzi wa wimbo mpya wa Msanii Linah - Ole - Temba akitoa shukrani zake za pekee.
Msanii Linah akitoa zawadi kwa Mtayarishaji wa Muziki na Msanii Nash Designer.
Picha mbali mbali za video mpya ya Msanii Linah iitwayo Ole-Temba aliyoifanyia nchini Afrika Kusini.
Kila mmoja akipata chakula katika hafla ya kumuaga Msanii huyo ilifanyika jana Julai 16, 2014 ndani ya ofisi za THT jijini Dar es Salaam.
Msanii Linah nae hakuwa nyuma kuikamilisha furaha yake.
Mazungumzo ya hapa na pale yakiendelea miongoni mwa wadau waliofika katika hafla ya kumuaga Msanii huyo ilifanyika jana Julai 16, 2014 ndani ya ofisi za THT jijini Dar es Salaam.
Shoo love za marafiki.
Mama na Mwana nao waliweza kufika katika hafla ya kumuaga Msanii huyo ilifanyika jana Julai 16, 2014 ndani ya ofisi za THT jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments: