Msanii wa Muziki wa Kizaki Kipya, Anasteria Sanga a.k.a Linah au muite Ndege Mnana anatarajia kuagwa leo Julai 16, 2014 majira ya jioni toka Tanzania House Of Talent (THT) na kuhamia kwenye kampuni itakayokuwa ikisimamia kazi zake ijuliakanayo kwa jina la No Fake Zone (NFZ).

Akizungumza na Kajunason Blog, Linah alisema mpaka anamshukuru Mungu alipofikia haina budi kuishukuru THT kwa kumlea tokea mwaka 2009 alipokuwa anatoka na wimbo wake wa Atatamani. 

Mpaka sasa kampuni hiyo imeshafungua milango kwa kumpa gari la kifahari ikiwemo mkataba ambao amesaini miezi miwili iliyopita pamoja na kurekodi nyimbo zipatazo tatu. Habari zaidi endelea kufuatilia hapa hapa...
Msanii Linah akiwa ameweka pozi kwenye mchuma wake.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: