Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Deogratius Munishi ‘Dida’, Shomary Kapombe, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mwinyi Kazimoto, Thomas Ulimwengu, Erasto Nyoni, John Bocco/Haroun Chanongo dk78, Mbwana Samatta/Simon Msuva dk83 na Mrisho Ngassa/Khamis Mcha dk57.

Msumbiji; Dario Khan, Momed Hagi, Zainadine Junior, Saddan Guambe, Francisco Mioche, Eduardo Jumisse/Isaac de Carvalho dk85, Elias Pelembe, Josemar Machaisse, Helder Pelembe, Almiro Lobo na Richard Campos. 
---
Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog, Dar es Salaam.

Timu ya Taifa Stars ya Tanzania imejikuta ikimalizia  vibaya hatua ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco, baada ya kuangukia pua ya sare ya 2-2 na Msumbiji.
 Katika mchezo huo, uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo Julai 20, 2014, mabao ya Stars inayofundishwa na Mholanzi Mart Nooij yalifungwa na kiungo wa Azam FC, Khamis Mcha ‘Vialli’ aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mrisho Ngassa.
 Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika huku kila timu ikitoka imeinamisha kichwa bila ya kufungana, baada ya timu kuingia kipindi cha pili, Msumbiji walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 47 kwa penalti iliyokwamishwa nyavuni na Elias Pelembe baada ya Kevin Yondan kucheza rafu kwenye eneo la hatari. 

Mcha aliisawazishia Stars bao hilo dakika ya 65 akimalizia kazi nzuri ya Thomas Ulimwengu.
 Mcha tena akaifungia Stars bao lililoelekea kuwa la ushindi dakika ya 71 kwa penalti, baada ya mabeki wa Mambas kumchezea rafu Mbwana Samatta kwenye eneo la hatari.

Stars iliongeza mashambulizi langoni mwa Msumbiji na kukosa mabao kadhaa ya wazi. Msumbiji walizinduka na kufanya shambulizi zuri lililowapatia bao la kusawazisha dakika ya 87 kupitia kwa Isaac Carvalho aliyetokea benchi pia.
Kwa matokeo, hayo Stars sasa itajitaji ushindi wa ugenini ili kusonga mbele, au sare ya kuanzia mabao 3-3, wakati wenyeji wanaweza kunufaika na sare ya 1-1 au 0-0. Ikiwa 2-2 tena, mshindi ataamuliwa kwa mikwaju ya penalti.

Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Deogratius Munishi ‘Dida’, Shomary Kapombe, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mwinyi Kazimoto, Thomas Ulimwengu, Erasto Nyoni, John Bocco/Haroun Chanongo dk78, Mbwana Samatta/Simon Msuva dk83 na Mrisho Ngassa/Khamis Mcha dk57.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: