Taasisi ya Faridas Foundation inatarajia kufanya uzinduzi wake rasmi siku ya tarehe 28/6/2014 siku ya jumamosi katika ukumbi wa crystal hall, blue pearl hotel, ubungo plaza kuanzia saa 6-12 jioni. 

Katika siku hyo taasisi itatoa misaada mbali mbali kwa walemavu ikiwemo baiskeli za walemavu, vyerehani, vifaa vya shule na vifaa vingine muhimu kwa walemavu ukiwa kama mdau au mtanzania unayeguswa na walemavu na ungependa kuhudhuria siku hyo maalumu kadi zinapatikana kwa mchango wa shilingi laki moja na kuendelea hii ikiambatana na chakula cha mchana vinywaji na burudani mbalimbali pia utakuwa umesaidia kuongeza idadi ya vifaa vitakavyotelewa kwa walemavu mbali mbali. Kutoa ni moyo sio utajiri. 


Endapo una kampuni au ungependa kushiriki kama kampuni au taasisi kwa kudhamini pia nafasi bado zipo wazi wasiliana nasi kupitia +255715186262 au email 
faridasfoundation@gmail.com
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: