Marehemu Lt. Col. Mstaafu Maurice Noel Singano enzi ya uhai wake.
Mwili wa Marehemu Luteni Kanali mstaafu, Maurice Noel Singano ukiwasili nyumbani kwa mtoto wake Mikocheni B jijini Dar es Salaam Alhamisi Juni 05.2014, kabla ya kusafirishwa kwenda mkoani Tanga kwa mazishi yaliyofanyika Ijumaa Juni 06.2014. Marehemu Mzee Singano alifariki Mei 31, mwaka huu huko katika Hospitali ya Appolo Chennai nchini India alikuwa akipatiwa matibabu baada ya kupata mshtuko.
Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu wakati wa kuuaga Mikocheni B jijini Dar.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. John Haule akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu wakati wa kuuaga Mikocheni B jijini Dar.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha siasa cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu wakati wa kuuaga Mikocheni B jijini Dar.
Jeneza lenye mwili wa marehemu likiingizwa katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Martha lililopo Mikocheni B jijini Dar, kwaajili ya misa kabla ya kuanza safari ya kuelekea Tanga kwa mazishi.
Maafisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kikosi cha 37 Tanga, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu wakati wa kuuaga nyumbani marehemu katika eneo la Sahare mkoani Tanga.
Mjane wa Marehemu, Bi. Maria Singano akilia kwa uchungu wakati akiuaga mwili wa mpendwa mume wake, nyumbani kwao katika eneo la Sahare mkoani Tanga.
Mtoto wa Marehemu, ambaye ni Mkuu wa Mahusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Bi. Beatrice Singano akilia kwa uchungu wakati akiuaga mwili wa mpendwa baba yake, nyumbani kwao katika eneo la Sahare mkoani Tanga.
Jeneza lenye mwili wa Marehemu, likiwa lemebebwa na askari wa JWTZ Kikosi cha 37, likitolewa nyumbani katika eneo la Sahare mkoani Tanga kwaajili ya kwenda kanisani na baadaye mazishi katika makaburi ya Bombo mkoani humo. Aliyeshika Msalana ni mototo wa Marehemu, Bw. Billy.
Jeneza lenye mwili wa Marehemu, likiwa lemebebwa na askari wa JWTZ Kikosi cha 37, likiwasili katika Kanisa Katoliki la Mt. Mathias mjini Tanga kwaajili ya misa kabla ya mazishi.
Padri wa Kanisa Katoliki la Mt. Mathias mjini Tanga akifanya sala kwa marehemu.
Jeneza lenye mwili wa Marehemu, likiwa lemebebwa na askari wa JWTZ Kikosi cha 37, likiwasili katika makaburi ya Bombo mjini Tanga kwaajili ya mazishi.
Shughuli za mazishi zikiendelea.
Shughuli za uwekaji wa mashada ya maua zikiendelea.
Askari wa JWTZ 37KJ wakifanya mazishi ya kijeshi, ikiwa ni pamoja na kupiga risasi kadhaa hewani.
Toa Maoni Yako:
0 comments: