Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe akishuhudia uharibifu kwenye moja ya madarasa ya Shule ya Msingi Weruweru iliyoko wilayani Hai, ikiwa ni sehemu ya ziara yake anayofanya pamoja na kamati yake ya Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo (CDF), kwa ajili ya kutathmini na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni kwake ili mfuko huo uweze kusaidia kuongeza nguvu za ujenzi. Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya mfuko huo alielezwa kuwa shimo hilo limekuwa likitumika na wananchi waovu kama 'mlango' wa kuingia na kutoka kwa ajili ya kuiba kuni zinazotunzwa katika chumba hicho cha darasa.
Mmoja wa Wanakamati wa Kamati ya Mfuko wa Maendeleo (CDF) Jimbo la Hai akipanga kuni katika moja ya madarasa ya Shule ya Msingi Shirimatunda iliyoko wilayani Hai, wakati Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Freeman Mbowe (Mbunge wa Hai), alipofanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo ambayo mfuko huo utasaidia kuongeza nguvu za ujenzi. Chumba hicho mbali ya kutumika na wanafunzi kwa ajili ya kusomea, pia kinatumika kama stoo ya kuni za kupikia chakula cha wanafunzi shuleni hapo, hali ambayo inadhihirisha kuwepo kwa mahitaji ya vyumba kwa ajili ya matumizi mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments: