Na Mwandishi Wetu, Dodoma. 

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, ametangaza Baraza lake la mawaziri kivuli 28 na naibu mawaziri 12, na kufanya baraza lote kuwa na mawaziri 40.

Katika baraza hilo la mawaziri linalojumuisha wabunge wanaotokana na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), mawaziri 25 wanatoka Chadema, 11 wanatoka CUF na NCCR-Mageuzi ni wanne.

Mawaziri kivuli walioachwa katika baraza hilo ni Sylvester Kasulumbay (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi), Highness Kiwia (Viwanda na Biashara) na Rose Kamili (Kilimo, Chakula na Ushirika).

Wengine walioachwa na Mbowe akasisitiza kuachwa kwao siyo kwa sababu hawawezi kazi bali ni kutaka kuwa na baraza la mawaziri dogo ni Sabrina Sunga (Naibu Waziri Maji).

Katika Baraza hilo, nafasi ya mnadhimu mkuu wa upinzani Bungeni iliyokuwa ikishikiliwa na Tundu Lissu (Chadema) sasa itashikiliwa na Mbunge wa Tumbe, Rashid Abdalah kutoka chama cha CUF.

Akitangaza baraza hilo Bungeni mjini Dodoma jana, Mbowe alisema Wizara ya Katiba na Sheria imeongezewa majukumu ya Muungano na waziri wake atakuwa ni Lissu na naibu wake ni Abdalah.

Pia amemteua Mbunge wa kuteuliwa na Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia ambaye anakuwa Waziri wa Fedha wakati Naibu wake atakuwa Christina Lissu kutoka Chadema.

Mawaziri Ofisi ya Rais ni Profesa Kulikoyela Kahigi (Utawala Bora-Chadema), Vicent Nyerere (Utumishi-Chadema) na Esther Matiko (Mahusiano na Uratibu-Chadema).

Ofisi ya makamu wa Rais itakuwa na mawaziri wawili ambao ni mchungaji Israel Natse kutoka Chadema atakayeshughulika na Mazingira na Naibu wake atakuwa ni Assah Othman Hamad (CUF).

Mnadhimu wa Upinzani Bungeni ndiye atakayeshikilia pia nafasi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Mazingira.

Mawaziri katika ofisi ya Waziri mkuu ni Pauline Gekul (Uwekezaji na Uwezeshaji-Chadema), Rajabu Mohamed Mbaruku (Sera, Uratibu na Bunge-CUF) na David Silinde (Tamisemi-Chadema).

Wizara ya Chakula, Kilimo na Ushirika itashikiliwa na Meshack Opulukwa (Chadema), Wizara ya Nishati na Madini atakuwa John Mnyika Chadema na Naibu wake “atakuwa Raya Ibrahim (Chadema).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: