Na Saimeni Mgalula, Mbeya

Watoto wawili wamefariki dunia katika ajari ya moto iliyo tokea Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoani hapa, baada ya nyumba waliokuwa wakiishi kuungua moto.

Tukio hilo lilitokea May 8 mwaka huu saa 1:30 jioni huko katika mtaa wa Mageuzi mji Mkongwe ambao upi katika kata ya Nsalaga, tarafa ya Utengule Usongwe mkoani hapa vivile aliwataja majina watoto hao ni Baraka Lackson (04) na Ester Lackson.

Aidha Mtoto Martin Kabwilile (09) alijeruhiwa kwa kuungua na moto miguuni na amelazwa katika hospitali Teule ya Ifisi na inadaiwa kuwa chanzo cha moto huo ni Mshumaa uliokuwa umewashwa na wahanga chumbani na wao kulala.

Pia Moto huo ulizimwa na Wananchi kwa kushirikiana Askari polisi na thamani halisi ya mali iliyo teketea bado kufahamika na Miili ya Marehemu imehifadhiwa katika hospitali hiyo teule kwasababu wakati wa tukio Wazazi hawakuwepo Nyumbani.

Akithibitisha tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ahmed Msangi na kutoa Wito kwa Wazazi walezi kuweka uangalizi wa kutosha kwa Watoto Wadogo

Kamanda Msangi aliwahamasisha wazazi kuchukuwa tahadhari kutokana na majanga yanayotokana na moto ilikuepuka majanga yanayoweza kujitokeza.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: