Wanachama wapya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakila kiapo cha utii cha hama hicho baada ya kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika mkutano wa hadharauliofanyika kwenye Uwanja wa Tgaifa katika Kata ya Bukene, wilayani Nzega leo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye wakiwapungia mikono wananchi baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Tgaifa katika Kata ya Bukene, wilayani Nzega leo.

 Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Taifa Kata ya Bukene, wilayani Nzega, wakiti wa mwendelezo wa ziara ya  katika Mkoa wa Tabora.

 Kianana akiwa na Mohamed Kashindye mmiliki wa shamba la kumwagilia la mpunga  alipoombwa kwenda kulikagua alipkwenda kukagua mradi wa maji katika Jimbo la Bukene, wilayani Nzega. Mkulima huyo alimuomba Kinana kufanya hivyo licha ya shamba lake kutokuwemo kwenye ratiba ya ziara ya kiongozi huyo. Kinana alikubali kukagua shamba hilo na kumpongoza Kashindye kwa kilimo hicho.

 Kinana akikashuka kwenye tanki  alipokuwa akikagua mradi wa maji wa Kijiji cha Itobo, Jimbo la Bukene, wilayani Nzega leo.

 Wahasimu wa kisiasa, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Husein Bashe (kushoto) akikumbatiana na Mbunge wa Jimbo la Nzega, Hamis Kigwangalah, walipokutana wakati Kinana akikagua mradi wa maji katika Kijiji cha Itobo, Jimbo la Bukene, Nzega.
 Kinana akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Taka Nzega, Samweli Buyigi alipokuwa akikagua chujio la maji mjini Nzega leo

 Akina mama wanachama wa CCM wakichanganya mchanga na simenti kwa ajili ya kufyatua matofali katika mradi wa akina mama uliofadhiliwa na Mbunge wa Viti MaalumMkoa wa Tabora, Munde Tambwe katika eneo la Ofisi za CCM Wilaya ya Nzega leo.
 Kinana akibeba tofali ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi wa matofali wa akinana mama wa CCM Wilaya ya Nzega. Kushoto ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nanuye akisaidia kufyatua tofari.
 Vijana wakitumbuiza kwa ngoma ya zeze walipokuwa wakimlaki Kinana katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Itobo, Jimbo la Bukene.
 Nape akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Itobo
 Wananchi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu Kinana akihutubia katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Itobo.
 Mbunge wa Jimbo la Bukene akibebwa na wananchi ikiwa ni ishara ya kupendwa wakati wa ziara ya Kinana katika jimbo hilo.
 Sehemu ya umati wa watu uliofurika kwenye mkutano wa CCM Kata ya Bukene .
Kinana akihutubia katika mkutano huo na kukemea kitendo cha wana Ukawa kuwatukana vingozi waasisi wa muungano. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: