Ofisa masoko mkuu wa kampuni ya kimataifa inayo shughulika na maswala ya ubora (SGS) Bwana Hemed Hamza akipatiwa maelezo na Ofisa masoko kanda ya Afrika kutoka Kampuni ya Hawle, Bwana Alois Ramaseder kuhusu vifaa vya mabomba ya maji safi na maji taka vinavyo tengenezwa na Kampuni ya Hawle ya Nchini Austria na anayeshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Prima Business Consulting KG ya nchini Austria Bwana Dietmar Steininger (amevaa suti nyeusi). Maonyesho hayo ya vifaa vya maji safi na maji taka pamoja na vifaa Gesi kutoka nchini Austria yanafanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam Tanzania. Picha zote na Chris Mfinanga.
Ofisa masoko mkuu wa kampuni ya kimataifa inayo shughulika na maswala ya ubora (SGS) Bwana Hemed Hamza akiwa anawafahamisha watengenezaji wa vifaa vya Gesi pamoja na Maji safi na Maji taka kutoka Nchini Austria kuhusu uingizaji Nchini vifaa vyenye Ubora Kushoto kwa bwana Hamza ni Eng Wolfgang Wachter kutoka Kampuni ya ELIN Wasserwerkstechnik (EWT) inayotengeneza Mita za kisasa za maji na gesi ya Nchini Austria anayefutia ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni OSTAP inayotengeneza mitambo ya maji machafu ya Nchini Austria, Eng Christopher Gierlinger na anayefutia ni Ofisa masoko kanda ya Afrika kutoka Kampuni ya Hawle, Bwana Alois Ramaseder.

Eng Artmann Haralld kutoka kampuni ya ELIN Wasserwerkstechnik (EWT) ya nchini Austria akitoa maelezo kuhusu Mita za kisasa za maji na gesi zinazotengenezwa na kampuni yake kwa baadhi ya wataalamu wa maswala ya gesi na maji waliofika katika maonyesho ya vifaa hivyo inayofanyika katika Hoeli ya Serena Jijini Dar es salaam Tanzania.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: