Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi (aliyeshika kipaza sauti) akisoma barua maalumu iliyotumwa kwa ubalozi wa Nigeria nchini Tanzania kuonesha wanaharakati hao kupinga utekaji wa wasichana uliofanyika Nigeria. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi (aliyeshika kipaza sauti) akisoma barua maalumu iliyotumwa kwa ubalozi wa Nigeria nchini Tanzania kuonesha wanaharakati hao kupinga utekaji wa wasichana uliofanyika Nigeria.Mkurugenzi wa WiLDAF, Dk. Judith Odunga, akizungumza kupinga ukatili uliofanywa kwa wanafunzi wa kike kutekwa na kitendo cha Jeshi la Polisi nchini Tanzania kuzuia maandamano hayo ya wanaharakati. Mkurugenzi wa WiLDAF, Dk. Judith Odunga, akizungumza kupinga ukatili uliofanywa kwa wanafunzi wa kike kutekwa na kitendo cha Jeshi la Polisi nchini Tanzania kuzuia maandamano hayo ya wanaharakati.Viongozi wakuu wa Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) wakipokea mabango yenye jumbe anuai za kupinga vitendo vya kikatili vilivyofanywa  na wanamgambo wa Boko Haram. Viongozi wakuu wa Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) wakipokea mabango yenye jumbe anuai za kupinga vitendo vya kikatili vilivyofanywa na wanamgambo wa Boko Haram.Baadhi ya wanafunzi wa kike na wanaharakati wakiandamana kupinga vitendo vya kikatili vinavyofanywa na kundi la wanamgambo wa Boko Haram. Baadhi ya wanafunzi wa kike na wanaharakati wakiandamana kupinga vitendo vya kikatili vinavyofanywa na kundi la wanamgambo wa Boko Haram.Baadhi ya wanaharakati na wanahabari wakisikiliza sauti za viongozi wakuu wa Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) mara baada ya kupokea maandamano ya wanaharakati na wanafunzi kupinga utekaji wa wanafunzi wasichana uliofanyika na kikundi cha wanamgambo wa Boko Haram. Baadhi ya wanaharakati na wanahabari wakisikiliza sauti za viongozi wakuu wa Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) mara baada ya kupokea maandamano ya wanaharakati na wanafunzi kupinga utekaji wa wanafunzi wasichana uliofanyika na kikundi cha wanamgambo wa Boko Haram.

MTANDAO Mtandao wa Mashirika Huru ya Kijamii (CSOs) nchini Tanzania pamoja na baadhi ya wanafunzi wa kike shule kadhaa za Sekondari jijini Dar es Salaam umefanya maandamano kupinga kitendo cha kikatili kilichofanywa na kikundi cha Boko Haram cha nchini Nigeri cha kuwateka wanafunzi wa kike na kuwashikilia.

Maandamano hayo ya ndani yaliyoshirikisha wanaharakati mbalimbali yamefanyika ndani ya viwanja vya TGNP Mtandao eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi wa mashirika yanayounda CSOs walipokea maandamano na kusoma barua maalumu yenye ujumbe wa kupinga utekaji uliofanyika na kuishinikiza Serikali ya Nigeria itekeleze matakwa ya watekaji ili wanafunzi waliotekwa waachiwe huru.

Akisoma barua hiyo kwa niaba ya CSOs, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Bi. Lilian Liundi alisema mashirika yao yanaotetea haki za wanawake na watoto yameamua kuungana na mitandao na wanaharakati wengine duniani kote kulaani kitendo cha kinyama cha kuwateka nyara wasichana wanafunzi zaidi ya 200 waliokuwa shuleni nchini Nigeria, tukio lililofanywa na wanamgambo wa kikundi cha Boko Haram.

Alisema mashirika hayo yametumia maadhimisho ya siku ya kimataifa ya familia ulimwenguni kulaani kitendo hicho cha kikatili na kuitaka Serikali ya Nigeria kuhakikisha inawajibikaji ipasavyo ili kuwarejesha mateka hao mara moja tena wakiwa salama.

CSOs wamelazimika kufanya maandamano hayo ya ndani baada yale ya kutaka kuandamana hadi Ubalozi wa Nigeria kuzuiwa na Jeshi la Polisi kwa sababu kadhaa. Hata hivyo baadhi ya askari polisi walikuwa pembeni mwa viwanja vya TGNP Mtandao katika huku zoezi la maandamano ya ndani likiendelea. Baadhi ya Mashirika yanayounda CSOs ni pamoja na TAMWA, TGNP Mtandao, WiLDAF, LHRC.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: