Meneja uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim, akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa kutangaza siku ya kukabidhi zawadi za washindi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Pamoja nae katika picha, wa kwanza kutoka kushoto ni Ofisa Matukio na Udhamini wa Vodacom Tanzania, Ibrahim Kaude, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura.
------
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Bingwa wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2013/2014 timu ya Azam FC itakabidhiwa kitita chake cha zawadi Sh 75 Milioni Mei 27 mwaka huu kutoka kwa mdhamini wa ligi hiyo kampuni ya huduma za mawasiliano ya simu za mkononi nchini ya Vodacom.

Aidha, pamoja na Azam fc, Vodacom itakabidhi pia zawadi za fedha kwa Yanga, Mbeya City na Simba waliomaliza msimu katika nafasi ya pili hadi ya nne.

Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim amesema tayari maandalizi ya tukio hilo litakalohusisha chakula cha jioni yameshakamilisha kwa kiasi kikubwa na kinachoendela sasa ni maandalizi ya mwisho ikiwemo kusambaza mialiko.

Mwalim amesema tukio hilo hilo litafanyika kwenye ukumbi wa JB Belmonte uliopo kwenye jengo la Golden Jubilee jijini Dar es salaam na kuwataka washabiki wa soka nchini kuaka mkao w akuhushudia tukio kubwa na la aina yake.

“Sasa tunatangaza rasmi kuwa Azam pamoja na timu na wachezaji wengine waliofanya vema katika maeneo mbalimbali wanaostahili kupata zawadi za fedha kutoka kwa mdhamini kuwa litafanyika Mei 27. Hii inafuatia kujiridhisha na maandalizi yote yanayohitajika.”

Mwalim amesema kuwa tukio hilo litarushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha AZAM ambao nao kwa upande wao wameshakamilisha maandalizi ya kiufundi kwa kiasi kikubwa.

Hii ni mara ya kwanza kwa tukio hilo kurushwa moja kwa moja kwenye televisheni.

Mwalim amesema kurushwa moja kwa moja kwa tukio hilo kunaendana na mambo mengi mazuri ambayo AZAM TV wanatarajia kuyarusha ukumbini na hata kwa watazamaji watakaofuatilia utoaji huo wa tuzo hizo ikiwemo rekodi za matukio mahiri ya wachezaji, vilabu na hata mashabiki kwa mechi za msimu wa 3013/2014

Mwalim amewapongeza AZAM TV kwa kukubali kwao kuwa mbia kwenye tukio hilo katika eno la matangazo na utayarishaji wa matukio ya kimichezo.

“Tunawapongeza na kuwashukuru AZAM TV kwa kukubali kuungana nasi kwenye tukio hilo, Vodacom ina amini kuwa maendeleo ya mpira wa miguu nchini yanahitaji ushiriki na mchanago wa wadau wengi zaidi na ndio maana wakati wote tumeweka milango ya udhamini wazi kwa wadau wanaopenda kufanya hivyo bila kuathiri vipengele vya msingi vya mkataba mkuu.”

Mwalim amewashukuru TFF na Bodi ya Ligi kwa ushirikiano wao mkubwa uliofanikisha kukamilka kwa maandalizi ya tukio hilo la utoaji zawadi na tuzo, ushirikiano ambao amesema unaendelea kuleta tija kwa familia ya mpira wa miguu hapa nchini hususan ligi kuu ya Vodacom.                                                                                                                                                                                                                                
Timu za Yanga, Mbeya City na Simba zilizomaliza nafasi ya pili hadi ya nne zitavuna 37M, 26M na 21M zote zikiwa na nyongeza ikilinganishwa na kiasi walichozawadiwa timu zilizoshika nafasi hizo msimu uliopita wa 2012/2013.

Wengine watakaovuna fedha kutoka Vodacom ni timu iliyoonyesha nidhamu (Sh. 16), mchezaji bora (5.2M), mfungaji bora (5.2M), mlinda mlango bora 5.2M), mwamuzi bora na mwalimu bora 7.8M kila mmoja.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: