Na Saimeni Mgalula, Mbeya.

Mkazi mmoja Aswile Andokisye (24) wa kijiji cha Nkuyu kilichopo Wilaya ya Kyela.ameshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kukutwa na bhangi kete 64 Zenye uzito wa Gram 320.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Msaidi Mwandamizi wa Jeshi la polisi Ahmed Msangi alisema kuwa Tukio hilo lilitokea may 15 mwaka huu saa 8 mchana huko tatika eneo la kata ya nkuyu Tarafa ya Unyakyusa Mkoani hapa.

Pia Kamanda Msangi alimalizia kwa kusema kuwa mtuhumiwa alikuwa ni mtumiaji na muuzaji,na taratibu za kisheria zinafanywa ilimtuhumiwa afikishwe mahakamani alisema Kamanda Msangi

Aliendelea kwa kutoa wito kwa jamii kuacha kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya kwani ni kinyume na sheria.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: