Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KLABU ya Ako Labamba ya jijini Dar es Salaam imejitosa kudhamini shindano la Miss Ubungo litakalofanyika mwezi ujao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja Miradi wa Kampuni ya AKO Group Ltd, Honesty Minde, alisema wameamua kudhami ni shindano hilo ili kusaidia klifanikisha.

Alisema wameamua kuwasaidia waandaaji wa shindano hilo ili kukuza sanaa ya urembo, wakiamini kuwa ndio dira ya maendeleo kwa Watanzania wote.

“Tuliamua kuwapa maeneo ya kufanya mazoezi pamoja na huduma nyingine muhimu kwa waandaaji na warembo wao.

“Naamini kwa pamoja tutafanikisha kwa vitendo mafanikio makubwa ya Miss Ubungo mwaka huu, ukizingatia kuwa ndio lengo letu,” alisema.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: