Meneja wa Bia ya Castle Lager, Kabula akiongea katika uzinduzi wa Mashindano hayo ngazi ya Mikoa inayotarajia kuanza mwishoni mwa wiki hii. Pembeni ni Mratibu wa Mashindano ya Perfect Six yanayoendeshwa na bia ya Castle Lager, Bw. Peter Zacharia 
Mratibu wa Mashindano ya Perfect Six yanayoendeshwa na bia ya Castle Lager, Bw. Peter Zacharia akiongea katika uzinduzi wa Mashindano hayo ngazi ya Mikoa inayotarajia kuanza mwishoni mwa wiki hii. Pembeni yake ni Meneja wa Bia ya Castle Lager.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Mashindano ya Mpira wa miguu ya Castle Lager Perfect 6, yanaanza rasmi ngazi ya mikoa wikendi hii katika mikoa Dar es Salaam na Morogoro. Mashindano hayo yatamalizika kwa kupata washindi kutokana na fainali kimataifa ambao watatembelea uwanja wa Camp Noun na kujionea FC Barcelona ikicheza na kujionea sehemu mbali mbali za historia ya timu hiyo katika ziara ambayo itagharimiwa kila kitu cha Castle Lager.

Akiongea jijini Dar es Salaam Meneja wa Bia ya Castle Lager, Kabula Nshimo alisema Mei 24 Jumamosi yatafanyika mabonanza manne kwenye mikoa ya Temeke, Ilala na Kinondoni na Morogoro. Washindi wa kila mkoa watachuana katika mashindano ya kanda na hatimaye kupata washindi watakaoshiriki kwenye fainali kitaifa.

Akitaja maeneo ambayo mashindano hayo yatafanyika, Nshimo alisema kwamba kwa wilaya ya Temeke bonanza litafanyika Jumamosi kuanzia saa sita mchana kwenye uwanja wa Mwembe Yanga ulioko Temeke, Ilala- Uwanja wa Rova Ashanti uliopo Msimbazi Center na Kinondoni – Uwanja wa CCM Mwinjuma uliopo Mwananyamala wakati huo Morogoro bonanza litafanyika uwanja wa Fire uliopo Morogoro Mjini.
Mashindano yataendelea siku ya Jumapili Mei 25 ambapo yatafanyika Kinondoni Uwanja wa Garden Uliopo Sinza, Ilala-Uwanja wa Rova Ashanti na Temeke-Uwanja wa Zakhem Mbagala.

Maeneo Mengine yatakayofanyika katika nyakati tofauti kwa wiki kadhaa ni pamoja na Moshi, Arusha, Musoma, Mwanza, Kahama, Iringa, Mbeya na Dodoma.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: