Mamba aliyekuwa akiishi kwenye makazi ya watu Kinondoni Block 41, jijini Dar es Salaam hatimaye leo May 4, 2014 ameuliwa kwa kupigwa na risasi zipatazo nne. Kwa mujibu wa shuhuda aliyekuwepo eneo la tukio alisema kuwa Mamba huyo amekuwa akiishi kwa muda mrefu licha ya Wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka husika.

"Leo ameuwawa Mamba ambaye alikuwa akitulaza kwa hofu maana alitokea kujichanganya kwenye makazi ya watu ndipo watu walipomshambulia na baadae ilibidi tupate msaada wa jirani yetu ambaye alikuwa na bastola  na kufanikiwa kumpiga risasi nne na kumuua.  Pamoja na kuuwawa kwa mamba huyu bado wakazi wa eneo hilo wanawasiwasi wa kuwepo kwa mamba wengine.

Historia ya Mamba:
Mamba huyu alikuwa akiishi katika bwawa 
bwawa dogo lililoko katika eneo la mpaka kati ya mtaa wa Kumbukumbu Block 41 na ule wa ADA Estate kata ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam kwa muda mrefu takribani miaka mitano.

Kwa nyakati tofauti wakazi wa jirani na eneo la Bwawa hilo, wameeleza kuwa mnyama huyo si wa kwanza na kwamba alishapatikana tena mwingine kaika kipindi cha nyuma na walipotoa taarifa kwa idara za mali asili, mnyama huyo alichukuliwa na kuhamishwa, lakini siku za karibuni ameonekana tena mwingine.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Kumbukumbu Block 41 Majeshi Shabani amethibitisha kuwepo kwa taarifa hizo ni vyema kuchukua tahadhari mapema kabla ya athari, na hasa kwa kuzingatia kuwa ni kinyume na utaratibu na ni hatari kwa wanyama kama hao kuishi katikati ya makazi ya watu ndani ya eneo la jiji.
Mamba akiwa amewekwa juu ya gogo ili wananchi wamwangalie vizuri katika kituo cha Osterbay jijini Dar. Picha zote na EMMA Mdau wa Kajunason Blog akishirikiana na Erick Mgema.
Mamba alikuwa amekomaa kukadiliwa anaumri wa miaka mitano...
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: