Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Askofu Mteule, Alen Legeza Siso, baada ya kumkabidhi Katiba na Kanuni za Kanisa la Methodist Tanzania, wakati wa Ibada Maalum ya Kuwekwa Wakfu (kusimikwa) askofu huyo, iliyofanyika kwenye Kanisa la Imanueli dhehebu la Methodox, Jimbo teule la Pwani na Mashariki lililopo Bunju Jijini Dar es Salaam, leo Mei 3, 2014. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia Waumini wa dini ya Kikristo wa Kanisa la Methodist Tanzania, wakati wa Ibada Maalum ya Kusimikwa Askofu Mteule Alen Legeza Siso, iliyofanyika kwenye Kanisa la Imanueli, Jimbo teule la Pwani na Mashariki lililopo Bunju Jijini Dar es Salaam, leo Mei 3, 2014.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Methidist Tanzania, Dkt. Mathew Byamungu, baada ya Ibada maalum ya kusimikwa Askofu Mteule, Alen Legeza Siso, (kulia) kuwa Askofu wa Jimbo la Mashariki na Pwani iliyofanyika kwenye Kanisa la Imanueli, Jimbo hilo lililopo Bunju Jijini Dar es Salaam, leo Mei 3, 2014.

 Askofu Mkuu wa Kanisa la Methidist Tanzania, Mathew Byamungu, akimsimika Askofu Alen Legeza Siso, kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Mashariki na Pwani, Makanisa ya Methodist Tanzania, wakati wa Ibada Maalum ya kuwekwa Wakfu Askofu huyo iliyofanyika leo Mei 3, 2014, kwenye Kanisa la Emanueli lililopo Bunju jijini Dar es Salaam.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimina na baadhi ya wachungaji wa Kanisa la Emanueli, Jimbo la Mashariki na Pwani, wakati alipowasili jimboni hapo kwa ajili ya kuhudhuria Ibada maalum ya Kusimikwa, Askofu Mteule, Alen Legeza Siso, jijini Dar es Salaam, leo Mei 3, 2014.



 Baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo waliohudhuria Ibada hiyo maalum ya kumsimika Askofu Mteule, Alen Siso. 


Makamu wa Rais wa Jamhiri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa Kanisa la Methodist Tanzania, Dkt. Mathew Byamungu, Askofu Mteule wa Jimbo la Mashariki na Pwani, aliyesimikwa, Alen Siso na baadhi ya wachungaji wa Kanisa la Emanuel, baada ya ibada maalum ya kusimikwa Askofu, Alen, leo Mei 3, 2014.  

Kikundi cha Kwaya cha Msasani, kikitoa burudani wakati wa Ibada hiyo. Picha zote na OMR
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: