NI kama naangalia movie vile ya kusisimua! Mamba amembeba mbuzi mgongoni ili kumvusha mto mkubwa. Lakini katikati ya safari yao, mamba kwa uroho wake atageuka na kumwambia mbuzi kuwa ana njaa sana! Aidha amuache kwanza asake chakula kisha waendelee na safari au amle yeye tu. 

Hapo mbuzi atajua cha kufanya. Aidha amdanganye mamba ili amrudishe alipotoka jambo ambalo ni gumu sana kwake, au wafanyiane umafia, mbuzi akitaka kujinusuru na kifo na mamba akitaka kupata msosi wa rahisi... Mfano huu ni sawa na Chama Cha Wananchi CUF na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema. 

CUF iliyokuwa dhaifu Bara imebebwa mgongoni na Chadema Bara ili kujijengea tena heshima kwa Watanzania na Chadema imebebwa mgongoni na CUF Zanzibar ili nao wapendwe na kuheshimika Visiwani jambo ambalo ni gumu mno kwao. Nia yao ni kuendelea na safari ya kisiasa ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2015. 

Wakajitia kuungana. Sawa, lakini itakapofikia kutangaza mtu wa kupambana na CCM hapo lazima wamwagane. Wote wanataka upresdaa. Wote wanautaka umakamu wa rais au Waziri Mkuu. Sasa hapo lazima tumjuwe nani mbuzi na nani mamba, wakati huo mfalme wa maji anawaona tu wanavyotoana macho, mmoja akijifanya ana njaa ya madaraka na mwingine kutaka kujinusuru ili chama chake kisife. Aha ha ha haaaaa. Kuelekea 2015 tutajionea mambo mengi sana ya kufurahisha na kuchukiza pia. 

Mtazamo wa Kambi Mbwana. Mei 13, 2014.
Mungu Ibariki Tanzania.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: