Hatuna sababu ya kujitetea kama BABA zetu shule zilikuwa chache, miundo mbinu mibovu, teknolojia ya kawaida sana na nafasi za kazi chache pia. Tutasingizia nini sisi vijana wa leo? Wazee wetu na hali ngumu zote walizopitia ila katu hawakuwa na sababu za kujitetea kila mmoja alijituma ili aweze kujikomboa. 

Je tumerithi wapi hii hali ya kuwalaumu wengine kwa matatizo yetu wenyewe? Mbona waliotuleta duniani hawakuwa na desturi ya kuwalaumu wengine kwa matatizo yao wenyewe? Nadhani tunapoteza nguvu nyingi katika mambo ya kufurahisha na kuburudisha miili yetu na mambo ya msingi ya kesho yetu tunayapuuza. 

#Kila kijana ajichunguze muda wake mwingi amepotezea wapi?# - Hakuna wa kuisumbukia kesho yako zaidi ya wewe mwenyewe. AMKA UIJENGE KESHO YAKO : 

Imetolewa na Counsellor Cannon Luvinga.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: