Kwenu Viongozi wa Jiji la Dar es Salaam, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar,  na Wakuu wa Wilaya zote Tatu, Meya wa Jiji la Dar, Mkurugenzi wa Jiji la Dar, Wakurugenzi toka Halmashauri zote tatu Kinondoni, Ilala na Temeke, Mameya wa Wilaya zote tatu, jamani Kiukweli nikiwa Raia mwananchi wa kawaida ninaguswa sana kuona kero kama hizi zipo zinatuzunguka halafu hakuna hatua yoyote nyinyi Mpo Ofisini Mnakula viyoyozi siyo ishu.

Wadau fanyeni kweli ili kuwanusuru wananchi wa jiji hili, adha ya foleni kutokana na Miundombinu kuwa Mibovu, suala la Uchafu japo mnakusanya Kodi zetu halafu mnatangaza Mwaka huu 2014 Mapato yameongezeka katika Jiji au Halmashauri lakini hizo Fedha zinazobaki katika Halmashauri kazi yake ni ipi??
Kwa maana mkisema mnazipeleka katika Vikundi vya Vijana hakuna, mkisema Viccoba vya wakina Mama napo Zero sasa tuwaeleweje jamani, nyie nanyi ni Mizigo mnakuwa kero, lawama siyo kuwapelekea Serikali Kuu kila siku wakati nyinyi wasaidizi Mpo au ndiyoo Ofisini na Ndiyo Mzee tu.

Maoni haya yametolewa na James Rock Mwakibinga.

Kama na wewe unakero yako inayokugusa toka pande zozote za dunia, usisite kuwasiliana nasi kwa anwani; cathbert39@gmail.com/0787999774
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: