Rais Jakaya Kikwete akizungumza kabla ya kuzindua rasmi huduma mpya ya M-pawa ya kuweka pesa, kutoa na kukopa kupitia simu ya mkononi kwa njia M-pesa inayotolewa kwa ushirikiano wa Vodacom Tanzania na Benki ya CBA jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Kikwete (wa pili kulia) akiwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa huduma ya M PAWA ambayo inamwezesha mteja kupata huduma za kibenki kwenye simu ya mkononi kwa njia ya M-pesa iliyozinduliwa kwa ushirikiano wa Vodacom Tanzania na Benki ya CBA. Kupitia huduma hiyo mteja wa M-pesa anaweza kuweka, kutoa na kukopa pesa.
 Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Vodacom Tanzania Balozi Mwanaidi Maajar mara baada ya kuzindua huduma mpya ya M-pawa ya kuweka pesa, kutoa na kukopa kwenye simu ya mkononi kwa njia M-pesa kwa ushirikiano na Benki ya CBA jijini Dar es salaam. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa CBA Tanzania Ndewirwa Kitomari Wengine kutoka kushoto ni Naibu Mwenyekiti wa CBA Group Muhoho Kenyatta, Mwenyekiti wa Bodi ya CBA Group Desterio Oyatsi, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza.
Rais Jakaya Kikwete (wa tatu kushoto)akiwa pamoja na kutoka kushoto Mwenyekiti wa CBA Tanzania Ndewirwa Kitomari, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Vodacom Tanzania Balozi Mwanaidi Maajar, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa, Mwenyekiti wa Bodi ya CBA Group Desterio Oyatsi na Naibu Mwenyekiti wa CBA Group Muhoho Kenyatta mara baada ya Rais kuzindua huduma mpya ya M-pawa ya kuweka pesa, kutoa na kukopa kupitia simu ya mkononi kwa njia M-pesa kwa ushirikiano na Benki ya CBA jijini Dar es salaam.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: